Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » VIRUS VYA ZIKA VIMEGUNDULIWA MOROGORO NA GEITA KWA MUJIBU WA WATAFITI, JE! WATANZANIA WANAUWELEWA WA KUTOSHA KUHUSU UGONJWA HUU?...BAADHI YA DONDOO ZAKE ZIKO HAPA ITAKUSAIDIA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Lisemwalo lipo na kama halipo basi laja, ndivyo unaweza kusema hivyo kulingana na misemo na nahau za wahenga walivyofikiri.

Mwaka mmoja sasa umepita tangu virusi hatari vya zika kutajwa kuingia Tanzania, lakini zilikuwa ni tetesi tu na baadae ikajulikana kuwa ni tetesi ambazo hazikuwa na umakini wa kuitoa habari hiyo lakii ni miaka miwili sasa imepita tangu ugonjwa huo kuanza kuwa tishio nchini Brazil na kusababisha kutishia michuano y aKombe la Dunia pamoja na Olimpiki iliyokuwa ikifanyika nchini humo.

Jana wakati nikiwa nyumbani kwangu nikitafakari nikajikuta nikitahamaki kasha kumfikiria mke wangu kama alikuwa mjamzito, nilipohakikisha siyo nikawafikiria marafiki zangu kadhaa na kujikuta nikitahamaki kuwa walikuwa na wake zao wenye ujauzito, nilipotaka kuwataarifu kwa njia ya simu nikakumbuka sikwenda kwa shayo kununua salio nikahamaki tena.

Lakini baada ya kufukilia kwa muda nikakumbuka kuwa mtandao wa Airtel ninaotumia unaweza kutumiwa kwa upande wa Facebook bila kujali una salio au la!
Nikazama na kuanza kuutumia kuwatumia washkaji zangu ujumbe juu ya nilichokisikia na nilipata shukrani nyingi sana kutoka kwao nikasuuzika moyo kwa kufanikisha hilo, lakini muda si mrefu nikapata wazo la kuujulisha umma wote wa kitanzania kufahamu kilichonishtua lakini salio bado likawa ni tatizo lakini sio sana nikaingia nikakopa mtandao husika kisha nikakaa na kuanza kuandaa kitu kisha nikaibuka nacho hiki kijimakala ambacho kwa kukisoma naamini utajifunza kitu kuhusu Ugonjwa huu wa zika…Karibu!!

Hapa nchini {Tanzania} Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR imethibitisha kugunduliwa kwa virusi vya Zika mkoani Morogoro na Geita.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Mwele Malecela, virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, mji ulioko Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania {Kanda ya ziwa}.

Utafiti huo ulifanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.

Dkt Mwele Malecela ameambia BBC kwamba kwa sasa serikali inaangazia kuzuia wajawazito wasiumwe na mbu ambao wanaaminika kueneza virusi hivyo.

Virusi vya Zika vimekuwa vikisababisha watoto kuzaliwa wakiwa na ubongo uliodumaa na vichwa vidogo katika mataifa ya Amerika Kusini na sana Brazil.

Mapema mwaka huu, serikali ya Tanzania iliwaagiza madaktari wote kuwa macho kuhusu hatari ya virusi hivyo mlipuko ulipotokea nchini Brazil.

Virusi vya Zika huenezwa sana na mbu ingawa kumeripotiwa pia visa vya watu kuambukizwa virusi hivyo kupitia kufanya mapenzi.

Haijabainika iwapo aina ya virusi vya Zika vilivyopatikana Tanzania ni vile ambavyo vimekuwa vikisababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo Amerika Kusini.

Virusi vya aina hiyo viligunduliwa kwa mara ya kwanza barani Afrika katika visiwa vya Cape Verde mwezi Mei mwaka huu.

Jina la virusi hivyo linatokana na msitu wa Zika, Uganda ambapo virusi hivyo vilitambuliwa kwa mara ya kwanza 1947.

Wengi wa walioambukizwa aina ya awali ya virusi walikuwa wakipatwa na homa ambayo si kali sana, mwasho na maumivu katika maungio.

Lakini kwa aina ya sasa, ambayo mlipuko wake ulianza mwishoni mwa mwaka 2015 nchini Brazil, dalili zake zimekuwa kali na virusi hivyo vinaaminika kusababisha kudumaa kwa ubongo na kasoro nyingine mwilini.

Lakini Homa ya ZIKA ni nini?

Homa ya Zika (kwa Kiingereza Zika fever) ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Zika, jamii ya jenasi Flavivirus.

Dalili zake zinafanana na zile za virusi vingine vya jenasi hiyo, kama vile Homa ya dengue au alfavirusi chikungunya, lakini ni afadhali kidogo na kwa kawaida zinadumu siku 4 hadi 7 tu. Asilimia kubwa (60–80%) hazina dalili za pekee.

Wagonjwa wenye dalili ya ugonjwa huu wana homa kidogo, conjunctivitis, maumivu ya muda kwenye jointi (hasa zile ndogo za mikononi na miguuni) na mwasho ambao mara nyingi unaanza usoni na kuenea katika mwili wote.

Pamoja na kwamba ugonjwa huo hauna dalili za kutisha, wataalamu wa afya wanauhusisha na tatizo la microcephaly kwa mimba za wanawake wanaopatwa, kama ilivyoonyeshwa na mlipuko wa mwaka 2015 nchini Brazil ambao mwaka 2016 unazidi kuenea barani Amerika.

Katika mlipuko uliotokea huko Polinesia ya Kifaransa kulikuwa na ongezeko la Guillain–BarrĂ© syndrome.

Ugonjwa unaenezwa na mbu wa jenasi Aedes, hasa Aedes aegypti, lakini pia A. africanus, A. coargenteus, A. luteocephala.

Pia zimethibitishwa habari za kwamba ngono inaweza kusababisha ambukizo, na vilevile uchangiaji wa damu na uzazi (wakati wa kujifungua).
Kuna wakati Fulani mnamo mwezi mei mwaka huu Wanasayansi nchini Brazil walisema kuwa virusi vya ZIKA ambavyo vimehusishwa na kuzaliwa kwa watoto wakiwa na vichwa vidogo huenda ni hatari zaidi kuliko ilivyofikiriwa awali.
Madaktari bingwa walikiambia kituo cha habari cha BBC kuwa virusi vya Zika vinaweza kuwa sababu ya kutokea kwa matatizo ya neva za fahamu kwa mwanamke mmoja mjamzito kati ya watano wanaoathiriwa na Virusi hivyo.
Madaktari wengi na watafiti sasa wanakubali kuwa kuna uhusiano kati ya mbu anayeeneza virusi na tatizo la watoto kuzaliwa na dosari kwenye ubongo.
Lakini wakati asilimia moja ya wanawake walioathiriwa na virusi vya Zika wakati wa ujauzito kuelezwa kuwa watapata watoto wenye vichwa vidogo, Madaktari nchini Brazil waliiambia BBC kuwa asilimia ishirini ya mimba zilizoathiriwa na ZIKA zitasababisha aina nyingine ya kuharibiwa kwa ubongo wa mtoto akiwa tumboni.
Kasi ya maambukizi katika baadhi ya sehemu nchini Brazil imepungua kutokana na elimu iliyotolewa kuzuia maradhi hayo, hata hivyo hati hati za kusaka chanjo ya kupambana na Virusi bado ziko katika hatua za awali, huku hatari ikiendelea kuwepo katika ukanda wa Amerika ya kusini.
#Njia 10 za kujikinga dhidi ya virusi vya Zika

Katika mataifa 20, ambapo virusi hivyo vinaaminika kuchangia kuzaliwa kwa watoto wenye vichwa vidogo, na hasa Brazil, tahadhari imetolewa.

Ni mlipuko wa maradhi ambao unaendelea, na Dkt Anthony Fauci, ambaye ni mtaalamu wa maradhi ya kuambukiza katika Taasisi ya Taifa ya Afya Marekani.

Kuenea huku kwa kasi kwa virusi vya Zika ndiko kwa karibuni zaidi kati ya magonjwa manne ya virusi yanayoenezwa na mbu mataifa ya Magharibi katika kipindi cha miaka 20, anaandika Dkt Fauci kwenye makala katika jarida la kimatibabu lathe New England Journal of Medicine.

Mlipuko huu unafuata mlipuko wa maradhi ya kidingapopo (homa ya dengue), virusi vya Nile Magharibi, na majuzi zaidi, chikungunya. Sawa na maradhi haya, virusi vya Zika pia huenezwa na mbu.

Lakini kinyume na virusi hivyo vingine, hakuna chanjo dhidi ya Zika. Je, ni njia gani iliyopo ya kukabiliana na virusi hivi?

1. Kutumia dawa au mafuta ya kufukuza mbu

Ushauri wa kwanza kabisa ni kuepukana na mbu. Kituo cha Kudhubiti na Kuzuia Maradhi (CDC) nchini Marekani kinapendekeza watu wajipake mafuta yenye kemikali za kufukuza mbu kama vile N, N-diethyl-meta-toluamide (DEET) au picaridin.

Mafuta haya yanafaa kujipakwa mara kwa mara, kwa kufuata maagizo kwenye mikebe, au mtu anapoanza kuumwa na mbu. Mtu anafaa kujipaka baada ya kujipaka mafuta ya kukinga ngozi dhidi ya miali ya jua.

Mafuta mengi ya kufukuza mbu ni salama hata kwa kina mama waja wazito, lakini ni vyema kutafuta ushauri wa daktari kabla ya kuanza kuyatumia.

2. Kuvalia mavazi ya kufunika mwili

Wataalamu pia wanakubaliana kwamba inafaa kuvalia mavazi yanayofunika mwili vyema. Mfano shati au nguo zenye kufunika mikono na pia suruali au long’i ndefu. Mavazi yanafaa kuwa mazito kuzuia mbu kufikia ngozi.

Katika baadhi ya mataifa, mavazi huwekwa dawa maalum aina ya permethrin, ambao hufukuza mbu.

Iwapo utajipaka mafuta ya kufukuza mbu, usijipake na kisha kufunika maeneo uliyojipaka kwa nguo unazovalia.

3. Kuzuia mbu kuingia nyumbani

Ikiwezekana, wataalamu wanawashauri watu walale ndani ya nyumba zilizojengwa vyema na kuwekwa kinga ya kuzuia mbu kuingia.

Usiku, lala Ndani ya neti yenye dawa.

Lakini usitahadhari usiku pekee kwani mbu aina ya Aedes aegypti, wanaoeneza virusi vya Zika, hupenda sana kuuma watu mchana.

4. Chunga mimea inayokua ndani ya nyumba

Ingawa ni muhimu kuzuia mbu kuingia, ni muhimu hata haidi kuzuia mbu kuzaana. Na mbu huhitaji maji.

Watu wanashauriwa kuchunga sana maeneo yenye maji yaliyosimama kwani huko ndiko viluwiluwi wa mbu huwa. 

Maeneo haya ni pamoja na mikebe, maeneo ya kuwapa mifugo na wanyama wengine lishe, jagi za kuweka maua, vibanda vya kufugia ndege na mimea ya kupandwa ndani ya nyumba.

Ni vyema pia kusafisha mifereji ya maji mara kadha kila wiki, mufunika matangi ya mali na vidimbwi la sivyo kuweka dawa ya krolini (krolini huwafukuza mbu).

Maji ambayo yametulia kwa zaidi ya siku tano yanafaa kutupwa kwa kumwagwa ardhi kavu, kwani viluwiluwi wa mbu watafariki baada ya maji kukauka. 

Kiasi kidogo tu cha maji kinatosha kwa viluwiluwi hao kukua kwa hivyo, ni vyema kuosha na kukausha vyema maeneo hatari.

5. Kufunika taka

Maeneo ya kutupwa taka mara nyingi huwa na maji na hutumiwa sana na mbu kuzaana.

Ili kuzuia hili, ni vyema kufunika taka, hasa katika mifuko ya plastiki.

Tairi kuukuu na vitu vingine vya ujenzi pia vinafaa kuwekwa vyema, kwani sana huhifadhi maji ambayo yanaweza kutumiwa na viluwiluwi wa mbu.

6. “Kunyunyizia dawa”

Maafisa nchini Brazil, ambako virusi vya Zika vimeenea sana, wanatafakari wazo la kunyunyizia maeneo yaliyoathiriwa na virusi hivyo dawa ya kuua mbu.

Hii inachukuliwa kama njia ya dharura kabla ya michezo ya Olimpiki, ambayo itaanza mjini Rio de Janeiro mwezi Agosti.

Hata hivyo, kuna utata kwani njia hii inaweza kuwa na madhara mengine kwenye mazingira na pia kuathiri afya ya wakazi.

7. Kudhibiti mbu

Serikali katika nchi kadha za Amerika Kusini tayari wameanza kampeni ya kuangamiza mbu wanaobeba virusi vya Zika kwa kutumia teknolojia.

Moja ya njia tata zinazopendekezwa ni kueneza mbu waliofanyiwa mabadiliko ya kijeneti ambao hawana uwezo wa kuzaana. 

Hili litapunguza idadi ya mbu na kuzuia ugonjwa huo kuenea.

Wengine wamejaribu mbinu nyingine, mfano jiji la Itapetim nchini Brazil. Maafisa mjini humo wanatumia samaki kuangamiza mbu huo.

Samaki hao hula mayai ya mbu na hivyo kuzuia kuongezeka kwa idadi ya mbu hao.

8. Vifaa ya kukabili mbu nyumbani

Maafisa wa serikali wanapojaribu kukabiliana na mbu kwa kiwango kikubwa, watu binafsi manyumbani pia wanatumia njia mbalimbali kukabili mbu.

Wanatumia vifaa mbalimbali vya kujikinga na kuwaua mbu. 

Mfano ni kutumia kifaa kinachoiga mwili na kutoa hewani ya kaboni dayoksaidi pamoja na joto, ili mbu waingie ndani wakidhani ni binadamu.

Mitambo mingine ya kunyunyiza dawa ya kuua mbu pia inatumiwa, lakini inapingwa na baadhi ya watu kwani inaathiri pia nyuki, vipepeo na wadudu wengine.

9. Kukwepa kusafiri

Wale wanaoishi maeneo ambayo hayajaathirika na virusi hivyo, wanajizuia kusafiri.
CDC imewashauri wanawake waja wazito nchini Marekani kuahirisha ziara zao Amerika Kusini na visiwa vya Caribbean kadiri wawezavyo.

Kituo hicho kimewashauri wanawake wanaopanga kusafiri maeneo hayo kutafuta ushauri wa madaktari kwanza.

Shirika la Afya Duniani (WHO), hata hivyo, halijaunga mkono ushauri huo wa CDC.
“Kwa kutumia ushahidi uliopo, WHO haipendekezi vikwazo vya usafiri au biashara kuhusiana na virusi vya Zika. 

Lakini kama tahadhari, mataifa mbalimbali yanaweza kutoa mapendekezo mbalimbali ya kiafya na kuhusu usafiri kwa raia wake, kwa kuzingatia utathmini,” WHO imesema.

10. Kuzuia kuenea

Mtu anapoambukizwa, hatua zaidi zinafaa kuchukuliwa kuzuia kuumwa tena na mbu wiki ya kwanza baada ya kuugua, CDC inasema.

Hii ni kwa sababu virusi vya Zika vinaweza kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mtu mwingine kupitia damu baada ya kuumwa na mbu.

Ingawa hatari ya kuenezwa kwa virusi hivi kupitia kujamiiana haijathibitishwa kisayansi, baadhi wanapendekeza watu watumie mipira ya kondomu hadi wiki mbili baada ya kupona.

Aidha, watu wachukue tahadhari kuepusha kuambukizwa virusi hivyo kupitia mate na majimaji ya mwili.

Je! Baada ya kugundulika kwa virusi hivyo hapa nchin tanzania, nini sasa hatua tunapaswa kuchukua? Kazi kwenu watanzania wenzangu lakini pia binadamu wenzangu nikimaanisha watu kutoka mataifa mengine nje ya Tanzania kusoma dalili na chanzo kasha jinsi ya kujikinga kama nilivyokuwekeeni hapo.

#Mtayarishaji na mchapishaji ni..Denice J. Kazenzele kwa msaada wa Bbcswahili.com pamoja na internet kwa ujumla.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / VIRUS VYA ZIKA VIMEGUNDULIWA MOROGORO NA GEITA KWA MUJIBU WA WATAFITI, JE! WATANZANIA WANAUWELEWA WA KUTOSHA KUHUSU UGONJWA HUU?...BAADHI YA DONDOO ZAKE ZIKO HAPA ITAKUSAIDIA

No comments :