Idara inayohusika na Masuala ya Sheria
Marekani iko kwenye mpango wa kurekebisha Sheria pamoja na kuwaachia
huru wafungwa 6,000 baada ya Magereza mengi ya nchi hiyo kuonekana kufurika Wafungwa kwa sasa !!
Moja ya sababu ambazo zimetajwa
kuchangia Magereza mengi kujaa ni ishu ya Sheria kali zilizowekwa
Marekani kwa Watuhumiwa wa Kesi za dawa za kulevya.
Kwenye idadi hiyo ya Wafungwa
watakaoachiwa wengi wao ni wenye Kesi za Dawa za Kulevya na hata kabla
ya kuachiwa pia kuna vitu vingi vitaangaliwa kuhusu usalama wa maisha ya
watu wengine nje baada ya Watuhumiwa hao kuachiwa.
Wafungwa hao wataanza kuachiwa kuanzia
October 30 mpaka November 02 2015… Mpaka mwisho wa mwaka 2014 Takwimu
zinaonesha kulikuwa na Jumla ya Wafungwa Milioni 1.56 kwenye Magereza ya
Marekani, huku Takwimu nyingine zikionesha Marekani ina Magereza mengi
zaidi kuliko idadi ya Vyuo vilivyopo.
No comments
Post a Comment