Tiketi za mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za
Kombe la Dunia chini Urusi mwaka 2018 kati ya Tanzania dhidi ya Algeria
ziataanza kuuzwa kesho Ijumaa katika vituo 10 viliyopo jijini Dar es salaam.
Magari maalumu yenye stika yataanza kuuza tiketi hizo
za mchezo kesho saa 2 kamili asubuhi mpaka saa 12 jioni, ambapo tiketi zinauzwa
kwa shilingi elfu tano (5,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani na rangi ya
machungwa, na elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C.
Vituo vitakavyotumika kuuza tiketi hizo ni ofisi za
TFF – Karume, Buguruni – Oilcom, Mbagala – Darlive, Mnazi Mmoja, Luther House –
Posta, Big Bone – Msimbazi, Ubungo – Oilcom, Makumbusho – Stand ya Daladala,
Uwanja wa Uhuru.
TFF inawaomba wadau, washabiki na watanzania kujitokeza
kwa wingi kununua tiketi za mchezo huo katika magari maalumu yatakayokuwepo
kwenye vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi
zisizokuwa halali.
Wakati huo huo Ubalozi wa Algeria nchini Tanzania,
umewataka waandishi wa habari wanaotrajia kwenda kuripoti mchezo wa marudiano
jijini Algiers siku ya jumanne, kuwasilisha maelezo ya chombo wanachofanyia
kazi pamoja na vifaa watakavyovitumia kwenye mchezo huo (camera, vinasa sauti)
kuwasilisha maelezo hayo leo Alhamsi kabla ya saa 9 mchana katika ofisi za
Ubalozi huo kwa ajili ya kupatiwa Accreditation za kufanyia kazi.
Matokeo ya mchezo wa jana Azam Sports Federtaion
Cup (ASFC), ni Mshikamano 0 - 1 Cosmopolitan,
No comments
Post a Comment