Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » HIZI HAPA HABARI ZA KIMATAIFA JIONI HII YA NOVEMBA 22/2015
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

kwa habari mbalimbali tembelea http://www.kazenzele1.blogspot.com  
Vyombo vya dola vinafuata vidokezi muhimu kwa nia ya kumkamata japo wanasema kuwa wamegundua washirika wengi mno wa njama kama hiyo.

Brussels 

Mikahawa na maeneo ya burudani kati kati ya mji wa Brussels nchini Ubelgiji yamebakia mahame baada ya utawala kuamri maeneo yote ya umma kufungwa mapema kutokana na tishio la mashambulizi.

mitaa ilibakia mahame huku polisi na wanajeshi wakionekana wakipiga doria na kuendesha misako katika maeneo yanayoshukiwa uwa maficho ya wahusika wa shambulizi la kigaidi lililotokea Ufaransa majuzi.

Mikutano ya hadhara pamoja na mikusanyiko yote ilipigwa marufuku.

Inaanimika kuwa mmoja wa washukiwa wakuu wa njama ya kuishambulia Paris Salah Abdeslam alitorokea Ubelgiji baada ya kufanya mashambulizi hayo.

Brussels ni mahame
Sasa vyombo vya dola vinafuata vidokezi muhimu kwa nia ya kumkamata japo wanasema kuwa wamegundua washirika wengi mno wa njama kama hiyo.

''Tunajua hata tukimkamata Salah Abdeslam tishio la ugaidi halitatoweka kwani sasa tumegundua kuwa kunahatari kubwa zaidi ya watu ambao wanaweza kutekeleza mashambulizi'' alisema waziri wa usalama wa ndani bwana Jan Jambon.

Waziri mkuu Charles Michel alisema kuwa kumekuwa na habari za uwezekano wa kutokea shambulizi sawa na lililotokea mjini Paris wiki iliyopita.

Serikali ya Ubelgiji huenda ikatoa tahadhari ya usalama baadaye leo Jumapili.

Rafiki zake Abdeslam, wameaimbia runinga moja ya Marekani kuwa wamezungumza naye kwa njia ya Skype na akawambia kuwa yuko Brussels akitafuta njia za kurejea Syria.

Treni za chini kwa chini zimesitisha safari zake mjini Brussels

Yamkini anashukiwa kuwa amejihami kwa ukanda wa vilipuzi.

Aidha serikali ya Marekani imewaonya raia wake wasiondoke majumbani mwao kwa hofu ya kutokea mashambulizi ya kigaidi.

Chanzo: bbcswahili
****************************************************************************

Germany

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatimiza miaka kumi madarakani hii leo.  Merkel ni kansela wa tatu wa Ujerumani baada ya vita vikuu vya pili vya dunia kusalia muda mrefu hivyo madarakani. Katika utawala wake, Merkel amefanikiwa kuigeuza Ujerumani kuwa na usemi katika jukwaa la kimataifa. 

Ameiongoza Ujerumani hadi kuwa mstari wa mbele katika kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kiuchumi na fedha barani Ulaya na kuchukua majukumu ya kuwa mpatinishi muhimu katika mzozo wa Ukraine pamoja na kusimamia sera yake ya kuwapokea maelfu ya wahamiaji nchini Ujerumani. 

Chini ya uongozi wake, Ujerumani imeimarika katika nyanja nyingi na anajulikana kwa jina maarufu Mutti au Mama kwa usimamizi wake thabiti. Wakati Merkel alipoingia madarakani mwaka 2005, idadi ya watu waliokuwa hawana ajira ilikuwa zaidi ya watu milioni 4.5 ikilinganishwa na miaka kumi baadaye ya utawala wake ni watu milioni 2.6 wasio na ajira Ujerumani. 

Merkel ambaye ndiye mwanamke wa kwanza kuwa Kansela wa Ujerumani hajatangaza nia ya kugombea muhula mwingine madarakani mwaka 2017 lakini anatarajiwa kufanya hivyo.  

Chanzo: Dwswahili 
**************************************************************************************************

Marekani na washirika wake wataiangamiza Islamic State.

Marekani

Rais Barack Obama amesema kuwa Marekani na washirika wake hawatalegeza vita vyao dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu wa Islamic State.

Akiongea kwenye mkutano wa nchi za kusini mashariki mwa Asia ASEA,mjini Kuala Lumpur bwana Obama amesema kwa Marekani itaendelea kuongoza vita dhidi ya wanamgambo hao na kuwapokonya ardhi walioitwaa kabla ya kuwaandama viongozi wake na kuiangamiza kabisa.

Obama amesema kuwa mashambulizi ya Paris hayatakubaliwa na Islamic State wataangamizwa.
Obama aliitaka Urusi kuelekeza jitihada zake katika kuiangamiza Islamic State.

''Hatutakubali watu tuliowashinda katika viwanja vya kivita kurudi nyuma yetu na kuwaua raia ambao 

hawana hatia katika mikahawa majumba ya sinema na watoto wetu'' alisema Obama.

'Hawa ni watu waoga wauaji ambao hata hawana utu''
''Angalia walichokifanya huko Paris, kwa hakika hatutawaruhusu waendelea kufikiria na kuota ndoto ya kuwa hiyo ni kawaida''

"sharti sote tufanye jambo la kuwatahadharisha Islamic State iliwasidhanie kuwa tumeogopa'' alisema Obama.

chanzo: bbcswahili

****************************************************************************************************** 

Bamako

Utekaji nyara katika hoteli ya Bamako unadhihirisha mapambano dhidi ya ugaidi yanakwenda mbali nje ya miji mikubwa ya Ulaya. "Miungano isiyo ya kawaida itahitajika," anasema Mkuu wa Idara ya Afrika ya DW Claus Stäcker. 

"Sheria ya Sunny 16": muda mfupi kabla mauaji ya kihole mjini Bamako jeshi la Ujerumani, Bundeswehr, lilituma taarifa ya kuchekesha yenye kichwa hiki cha habari kuhusu kozi ya upigaji picha kwa ajili ya maafisa wa habari wa Mali. Siku moja baadaye, hakuna aliyekuwa akicheka. 

Wanamgambo wenye misimamo mikali ya dini ya kiislamu wametuma tena ishara nzito iliyo wazi kabisa - ishara kwamba wako tayari na wana ari ya kuendelea na kampeni yao bila huruma, na hasa zaidi baada ya athari walizozisababisha mjini Paris. "Mnaonesha ishara za udhaifu na kutokuwa na uhakika," walionekana wakisema. "Ushindi wetu unaongezeka."

Paris, Ankara, Beirut, Sharm el-Sheikh na Bamako, na Yola na Kano eneo la kusini: tukichora msitari kati ya maeneo yaliyokumbwa na mashambulizi ya umwagaji damu, tunafahamu kile ambacho jeshi huita ulingo wa moto. Eneo hilo ambalo si salama, linalotawaliwa na itikadi kali na mizozo, linakaribia kuizunguka Ulaya.

Miaka 24 iliyopita, mwanajeshi wa cheo cha juu wa jeshi la Ujerumani Bundeswehr, Inspekta Jenerali Klaus Naumann, tayari alionya juu ya "ukanda wa mzozo kutoka Afghanistan hadi Morocco". 

Wakati huo wengi walidhani alikuwa tu ni afisa wa jeshi mwenye mikakati aliyetia chumvi hatari iliyokuwepo. Kauli ya Naumann wakati huo kwamba umwagaji damu si lazima uwe mwiko kwa wanajeshi wa Ujerumani yenyewe ilivunja mwiko.

Leo ulingo wa moto uko kilomita kadhaa kutoka Ulaya, na eneo ambalo haliruhusiwi kuwa na shughuli za kijeshi kati ya Mali na Libya ni dogo kuliko eneo kubwa lenye mchanga na ukiwa la Sahara linavyotaka tuamini. Mataifa ya magharibi yamefaulu kuwaondoa viongozi wa kiimla, lakini pamoja na viongozi hao yameuondoa ukuta wa moto ulioilinda Ulaya.

Utekaji wa hoteli ya Radisson Blu, inayoelezwa kuwa mojawapo ya hoteli zinazolindwa vizuri katika mji mkuu wa Mali, Bamako, hasa ulikuwa ukiilenga Ufaransa, ambayo iliiepusha nchi hiyo kutokana na kitisho cha kusambaratika kwa hatua yake ya kuingilia kati kijeshi mwaka 2013 na hivi karibuni ikafaulu kuwaangamiza viongozi kadhaa wa kigaidi.

Lakini shambulizi la Bamako lilielekezwa pia kwa washirika wa Ufaransa na mtindo wa maisha wa nchi za Magharibi. Kama ilivyotokea katika mashambulizi ya mjini Paris, washambuliaji walikuwa wakitoa ujumbe wa msingi, kufuata nadharia ya mauaji makubwa ya kiholela. Na wanajeshi wa Ujerumani - ambao hivi sasa wako Mali kama wakufunzi - wamenasa katika balaa hilo.

Mashambulizi ya Paris yanaonekana yameimarisha ari ya wapiganaji wa jihad kumwaga damu. Hakuna sababu kuamini kwamba aina fulani ya kamandi ya kimataifa ya kundi la Dola la Kiislamu mjini Raqqa nchini Syria unaratibu mashambulizi katika jangwa la Sahara na eneo la Sahel kupitia simu, telegram yaani app ya kutuma ujumbe wa siri kwa haraka au hata michezo ya kompyuta. 

Masuhuba hawahitaji mawasiliano ya simu kufanya jambo fulani. Tabia zao zinafanana. Hakuna tofauti yoyote wakijiita "The Sentinels" (Al-Murabitoum) "Defenders of the Faith" - "Walinzi wa Imani" (Ansar Dine) au hata Dola la Kiislamu.

Chanzo: bbcswahili
************************************************************************** 

Algers

Serikali ya Algeria imefunga mipaka yake na nchi za Mali na Libya kufuatia shambulio la kigaidi la siku ya Ijumaa katika mji mkuu wa Mali Bamako. 

Taarifa kutoka Algiers zinasema kuwa, serikali ya Algeria imechukua hatua hiyo ya kufunga mipaka yake na majirani zake Mali na Libya mara tu baada ya kutokea shambulio hilo mjini Bamako ambalo limepelekea watu wasiopungua 27 kuuawa. 

Taarifa ya serikali ya Algeria imeeleza kuwa, mbali na kufunga mipaka hiyo, pia imechukua hatua za kuimarisha usalama katika maeneo ya mipaka yake na nchi hizo ili kuzuia upenyaji tarajiwa wa wapiganaji wa makundi ya kigaidi.

Mkuu wa majeshi ya Algeria amewaambia waandishi wa habari kwamba, usalama umeimarishwa katika mipaka ya nchi hiyo na Mali na Libya. 

Ripoti zaidi zinasema, serikali ya Algeria imewaweka katika hali ya tahadhari askari elfu hamsini ambao tayari wametumwa katika mipaka ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Chanzo: iribswahili 
******************************************************************************

Bagdad

Milipuko kadhaa imeutikisa mji mkuu wa Iraq Baghdad na taarifa za awali zinasema kuwa, watu wasiopungua 10 wamepoteza maisha yao. 

Vyombo vya usalama na duru za hospitali zinasema kuwa, kwa uchache watu 10 wamepoteza maisha yao na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia milipuko tofauti na ufyatuaji risasi uliotokea mjini Baghdad na katika viunga vya mji huo. 

Polisi ya Baghdad imetangaza kuwa, mlipuko wa kwanza ulitokea katika soko moja mjini humo katika eneo la al-Forat. 

Aidha vyombo vya usalama vya Baghdad vinasema kuwa, katika tukio jingine, watu wasiojulikana wakiwa na silaha wameshambulia kituo kimoja cha upekuzi katika mji wa Yusufiya uliopo umbali wa kilomita 40 kutoka katika mji mkuu huo. 

Wakati huo huo jana kulitokea mlipuko wa bomu la kutegwa barabarani katika eneo la Hur lililoko kusini mwa Baghdad na kupelekea kuuawa polisi mmoja.

Chanzo: iribswahili 
********************************************************************************************************

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / HIZI HAPA HABARI ZA KIMATAIFA JIONI HII YA NOVEMBA 22/2015

No comments :