Hayo yamebainishwa na mratibu wa maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika mikoa ya kanda ya kaskazini afande Grace Lyimo na kusema kuwa matukio hayo yanaonekana kuongezeka kutokana na jamii kuwa na muamko wa kutoa taarifa hizo kwenye vyombo vya kisheria.
CHANZO:Itv Tanzania
*******************************************************************
IRINGA
Chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa mjini kimekanusha kufutwa kwa kesi yao dhidi ya mkurungenzi wa manispaa hii pamoja na mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji PETTER MSINGWA.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa CCM wilaya ya iringa mjini ELISHA MWAMPASHE amesema kuwa taarifa zilizosambaa sehemu mbalimbali sio za kweli.
“Nimekuwa nikipigiwa simu nyingi toka jana nikipewa taarifa kuwa kesi yetu imetupiliwa mbali na imeenea sana kwenye mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali ukweli ni kwamba kesi ya uchaguzi namba tano ya 2015 haijafutwa”alisema Elisha mwampashe.
Mwampashe ameongeza kuwa kesi hiyo bado haijapangiwa siku ya kusikilizwa wala kupangiwa jaji wa kuendesha kesi hiyo hivyo anashangaa kuaona taarifa zinazendelea kuenena mitaani
“Ifahamike kuwa mahakamani kuna shauri la msingi ambalo lilikuwa na kupinga
matokeo na kuna shauri dogo namba 28 la mwaka 2015 ndio lilikuwa
likizungumziwa jana kwa lengo la kuomba kupunguziwa dhamana kutokana na sheria kuruhusu kufanya hivyo” alisema Elisha Mwampashe.
matokeo na kuna shauri dogo namba 28 la mwaka 2015 ndio lilikuwa
likizungumziwa jana kwa lengo la kuomba kupunguziwa dhamana kutokana na sheria kuruhusu kufanya hivyo” alisema Elisha Mwampashe.
Mwampashe amemalizia kwa kuwataka wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi kuendelea kuwa na subra kwa kuwa haki yao ya msingi itapatikana mahakani na kuwasii wananchi wanaopotosha taarifa hizi.
Kwa upande wake Fredrick Mwakalebela aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la iringa mjini amesema kuwa shauri lilofutwa ni la kuomba kupunguziwa pesa ya dhamana.
“Nilikuwa kimya kutokana na kufatilia swala hili kimya kimya kwa lengo la kupata haki yangu ya msingi ambayo nimenyang’anywa na mkurugezi wa manispaa ya iringa pamoja na mchungaji petter msingwa” alisema Fredrick mwakalebela
Mwakalebela amemalizia kwa kusema kuwa kesi hiyo inaendeshwa naye pamoja na chama cha mapinduzi kwa kuwa chama ndio kilichompa nafasi ya kugombea
ndio maana kila kitu anachokifanya chma lazima kijue juu ya kesi hivyo.
ndio maana kila kitu anachokifanya chma lazima kijue juu ya kesi hivyo.
Ilitolewa Taarifa Kuhusu kutupiliwa mbali kwa shauri ya dhamana ya kesi ya ubunge Iringa Mjini Msajiri wa Mahakama kuu Iringa Bi Ruth Masamu amesema kesi ya aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo La Iringa Mjini Fredrick Mwakalebela alitoa ombi la kuomba kupunguziwa dhamana kutoka milioni kumi na kushuka angalau kwa kiasi kidogo.
Hii ni kutokana na vifungu vya sheria kuruhusu kuomba ombi hilo na mahakama kulikataa na kumtaka aongeze mtuhumiwa ambaye ni mwanasheria wa serikali kwenye kesi yake kwa gharama hiyohiyo.
Hivyo uvumi uliotolewa jana kwamba kesi imefutwa si kweli kwa sababu mpaka sasa kesi bado haijapangwa wala kuanza kusikilizwa.
CHANZO: fullshangwe
*******************************************************************
DAR ES SALAAM
Mkurugenzi mkuu wa Bohari kuu ya dawa nchini Bwana Laurean Rugambwa amesema agizo la rais Dokta.John Magufuli kufugwa vitanda katika wodi ambazo hazina vitanda katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili agizo hilo limetekelezwa kwa asilimia mia moja baada ya ofisi za bunge kutoa shuilingi milioni 251 kwa ajili ya kununua vitanda vipya pamoja na magodoro na kumshiru rais kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi zake anazozitoa kwa manufaa ya wananchi.
CHANZO:Itv Tanzania
*************************************************************
ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohmaed Shein amendelea na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ambapo amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa mji mpya unaojengwa huko Fumba wilaya ya Magharibi.
CHANZO:Itv Tanzania
*****************************************************************************
DAR ES SALAAM
Matumizi mazuri ya rasilimali inayopatikana katika eneo husika kama itaendelezwa kwa kushirikina na serikali pamoja na viongozi wa eneop husika ikiwemo Kyerwa na Karagwe imeelezwa kuwa itasaidia kundi kubwa la vijana kupata ajira na kukuza pato la taifa pia.
Hayo yamesemwa na wabunge wapya wa Kyerwa na Karagwe jijini Dar es Salaam wakati wakielezea mikakati yao ya kusaidia kuharakisha maendeleo ya pamoja katika majimbo yao kwa kushirikiana na wakazi wa maeneo hayo wanaoishi jijini Dar es Salaam.
CHANZO:Itv Tanzania
****************************************************************
GEITA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeahirisha shughuli za mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo na kupeleka mahakamani shauri la kuomba kibali cha kuuaga mwili huo.
Uamuzi huo unachukuliwa baada ya jeshi la polisi mkoani Mwanza kushikilia msimamo wa kutofanyika mikusanyiko katika viunga vya jiji la Mwanza.
Awali shughuli za kuuaga mwili huo zilitakiwa kufanyika jumamosi hii jijini Mwanza na jumapili mkoani Geita na mazishi yangefanyika jumatatu Novemba 23 katika kijiji cha Kikobe mkoani Geita
Mvutano huu kati ya jeshi la polisi na chama hicho unawalazimu viongozi wakuu wa CHADEMA kuitisha mkutano na waandishi wa habari kutoa tamko na hatua wanazotarajia kuzifanya.
Baada ya kuwasili kwa viongozi hao, tamko rasmi linatolewa na mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe na kueleza kupeleka shauri hilo makamani ili kupata tafsiri ya kisheria
Aidha anaeleza masikitiko ya chama hicho juu ya hatua ya jeshi la polisi kuzuia shughuli za kuuaga mwili wa marehemu Mawazo katika uwanja wa wazi na ofisi ya kanda jijini Mwanza
Tamko hilo linaungwa mkono na baadhi ya viongozi wa CHADEMA pamoja na baba mlezi wa marehemu Mawazo ambaye pia amekubaliana na uamuzi unaotaka kuchukuliwa na chama hicho.
Mvutano huu umedumu kwa takribani siku tatu sasa na jeshi la polisi bado linaendelea kufanya doria katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza ikishikilia msimamo wake wa kupinga kufanyika kwa
mikusanyiko zaidi katika shughuli ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita Alfonce Mawazo aliyeuawa kwa kushambuliwa na mapanga mkoani humo.
chanzo:Startv
**********************************************************************
NJOMBE
CHAMA cha demokrasia na maendeleo Chadema, Jimbo la Njombe kusini
kimesema kuwa kimefungua kesi ya kupinga matokeo katika mahakama kuu ya
Tanzania kanda ya Iringa, na kuwashitaki Mgombea wa CCM, Mwalongo,
Mwanasheria wa serikali, na msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani Njombe, Leo, baada ya kufungua kesi hiyo
aliye kuwa Mgombea ubunge jimbo la Njombe Kusini Emmanuel Masonga
amesema kuwa wameamua kufungua kesi hiyo baada ya kujiridhisha ushahidi
walionao utawawezisha kushinda kesi yenye namba 6/2015.
Masonga
amesema kuwa wameanda wanasheria wa kutosha ambao watasimamia kesi hiyo
na kuwa watatajiwa siku ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo baada ya
kufanyiwa tathimini ya gharama ya uendeshaji na kuhakikishiwa ulinzi wa
gharama za kezi.
Amewaambia waandishi wa habari
kuwa ushahidi na vielelezo vyote tayari wanavyo kwaajili ya kuvitoa
mahakamani na kuwa hawata weza kuviweka wazi kwa kuwa tayari ni mari ya
mahakama kwa sasa tangu wafungue kesi na kuwa vikionyeshwa vinaweza
kuwapa ushindi wapinzani wao.
Amesema
kuwa mahakama inaenda kumtangaza mshindi baada ya kushinda kesi hivyo
wakazi wa mkoa wa Njombe wakae tayari kuyapokea matokeo.
Aidha
mwenyekiti wa kamati ya kusimamia kesi hiyo Emmanuel Filangali amesema
kuwa wameamua kuita waandishi wa habari kuwajulisha pale walipo fikia
baada ya kwa mara ya mwisho kufikia maamuzi ya kufungua kesi mahakamani.
***************************************************************************
No comments
Post a Comment