Habari kamili.
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imebomoa nyumba 96 zikiwemo ofisi za umma katika kijiji cha Kigwe wilayani Bahi Dodoma ambapo watu zaidi ya 360 hawana mahala pa kuishi huku ikiacha hasara kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa wahanga wa mvua hiyo wamesema ilianza jioni ya siku
ya jumatatu na kuendelea kwa muda mrefu huku upepo mkali ulioambatana
nayo ukiezua mabati na kubomoa nyumba ambapo tukio hilo limewaacha
katika mazingira magumu kwani wanakosa makazi na chakula hawana kutokana
akiba yote waliokuwa nayo kuharibika.
Miongoni mwa wahanga wa tukio hilo ni walimu wa shule ya sekondari
ya Kigwe ambao nyumba yao iliezuliwa mabati na mara baada ya kutokea
waliwasiliana na uongozi wa elimu wilaya lakini katika hali ya
kushangaza walimu hao wanadai afisa elimu wa wilaya hiyo akiwataka kutoa
pesa zao mifukoni kukarabati nyumba ambapo wanahoji mfuko wa maafa wa
wilaya una kazi gani.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Kigwe Mgwala Manala
Songola amesema tayari kamati ya maafa ya kata hiyo imefanya tathmini ya
madhara yaliyotokana na mvua hiyo huku akibainisha kuwa baadhi ya
wahanga wamehifadhiwa kwenye jengo la shirika lisilo la serikali la
Kisedet kusubiri taratibu zingine za msaada.
No comments
Post a Comment