TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Freeman Mbowe amesema kuwa hawatashiriki shughuli ya kuapishwa kwa Dk. John Pombe Magufuli inayotarajiwa kufanyika Alhamis, Novemba 5, 2015.
Kauli hiyo ya Mwenyekiti Mbowe aliyoitoa leo, imekuja wakati kukiwa bado kuna sintofahamu kubwa miongoni mwa Watanzania kuhusu mchakato wa uchaguzi hususan upigaji kura, ukusanyaji na ujumlishaji wa matokeo ulivyofanyika hasa katika nafasi ya urais.

"Hatutahudhuria shughuli hiyo ya kumwapisha Magufuli. Tumekubaliana
wote kwenye UKAWA, ndani ya CHADEMA, viongozi wetu, wabunge wetu wote
hawatahudhuria uapishwaji wala sherehe.
"Tumetoa wito kwa wananchi wote, Watanzania wote, wapenda mabadiliko na wapenda haki wote kwa ujumla kutohudhuria shughuli hiyo," amesema Mwenyekiti Mbowe.
Mwenyekiti Mbowe amesisitiza kuwa UKAWA, wapenda mabadiliko wote na Watanzania wapenda haki hawakubaliani na wanapinga mchakato wa uchaguzi hususan matokeo ya urais ambayo, kwa mujibu wa Katiba ya Nchi aliyosema ni mbovu, yakishatangazwa hakuna haki ya kuyapinga katika mahakama yoyote ile.
"Tunataka nchi na dunia nzima ijue wazi kuwa hatukubaliani na mchakato wa uchaguzi hasa matokeo ya urais ambayo kwa mujibu wa Katiba yetu mbovu, Mwenyekiti wa Tume akishatangaza hakuna mahali pa kuyapinga."
"Matokeo ya ubunge au udiwani yanaweza kupingwa mahakamani, lakini kwa matokeo ya urais Katiba yetu mbovu inawafunga mikono na miguu Watanzania wote ambao wangependa waone haki imetendeka katika nafasi hiyo," amesema Mwenyekiti Mbowe.
"Watawala wamechezea haki ya Watanzania kupiga kura. Kura zimehesabiwa kama karatasi za kawaida tu. Hujuma dhidi ya matokeo ya wagombea wetu imehujumiwa waziwazi. Safari hii hujuma hazikuwa kificho tena.
Kila mtu amejionea matokeo yaliyokuwa na Jaji Lubuva si yale ambaye yalikuwa yamebandikwa vituoni. Hayakuwa na uhalisia na matokeo yaliyokusanywa na mawakala.
Uchaguzi umefanywa kama ni jambo lisilokuwa na maana yoyote. Hiyo ni hatari sana kwa taifa lolote linalotaka kukuza demokrasia kama mojawapo ya nguzo za maendeleo. Hatuwezi kukubali kufika huko," amesema Mbowe.
Aidha, Mwenyekiti Mbowe ameongeza kusema kuwa vyama vinavyounda UKAWA vimeitisha kikao cha Wabunge wateule wote wa vyama hivyo ambao watakutana Alhamis, saa 4 asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Imetolewa leo Jumatano Novemba 4, 2015 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Coments za watumiaji wa Facebook

117 people like this.
Comments
15 of 95
George Kulwa Kama
ni Kweli basi Lowasa atakuwa kawamaliza UKAWA na mimi rasmi kesho
nachukua kadi ya CCM ili niutoe mchango wangu kuijenga nchi yangu
kuputia CCM tanzania sio lowasa na Lowasa hawezi kuwa tanzania
Doyo Hasan Doyo Itasaidia Nini
Respicius Joseph mkapimwe kama hamuwezi kuamini kwamba mmeshindwa basi kuna shida ndani yenu Mgufuli ndiye raisi jaman amin
Enatha Lutha lkn ninaimani watabaki nyumbani wakitazama tv zao na kushudia rais wetu mteule akiapishwa
Seiph Akili tumeshawazowea mbona hata 2010. hawakuwepo na hakuna kilicho halibika
Juma Ndaro Mkisusa Wenzenu Tunakula - Aibu Yenu Aibu Yao!
Nzellah Nzellah Kudondoka kwa nyasi (jani ) moja ktk nyumba hakuifanyi nyumba hiyo kuvuja.
Meshack Festo Huo n umbulula kutokuhudhiria hakuna maana yoyote
Shafiyu Hamad mbowe
acha ujinga kama unataka demokrasia kwanza ijenge kwenye chama chako
kwani haipo kabisa kwani uteuzi wa mgombea uraisi uri ufanya mwenyewe
arafu eti una dai demokrasia tz!!
Ally Ibn Walid ccm chaguo letu wenyewe tuipenda wenyewe acha waisome namba kina mbowe
Alex Gideon Alafu
kesho watakuja hapa watasema hooo katika hotuba yake leo ametusema
sana, sasa umeona wapi kawasema wakati mmesema hamtaangalia kuapishwa
kwake?
Mwanja Ibadi hapa kazi tu
Jackline Anthony Wajinga na viroba wanapelekeshwa na xhadema mbowe ana zake uarabunii
Write a comment...
No comments
Post a Comment