Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Uganda kwenye sehemu ya pili ya ziara yake Afrika.
Papa amelakiwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.Baadaye, Papa anatarajiwa kuelekea ikulu ya Rais mjini Entebbe, kisha ahutubie maafisa wa serikali na mabalozi humo ikuluni.
Baadaye atawahutubia walimu.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pia yumo nchini Uganda kukutana na Papa Francis.
Mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga anasema Vatican imevutiwa na ukosefu wa usalama pamoja na uhusiano kati ya Sudan na Sudan Kusini.
Wawili hao watakutana katika ikulu ya rais wa Uganda mjini Entebbe.
Papa Francis atakuwa Uganda hadi asubuhi ya Novemba 29. Bofya hapa kupata ratiba kamili ya ziara yake.
No comments
Post a Comment