Unapopitia blog hii utapata taarifa mbalimbali za kitaifa kimataifa,michezo na burudani,picha na vituko vya hapa na pele lakini pia usisahau video mbalimbali pamoja na makala tofauti tofauti ....tembelea >>> KAZENZELE1.BLOGSPOT.COM
NAMIBIA
Namibia imeanza kuandaa mazingira ya kujiondoa kwenye Mkataba wa Roma uliobuni Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, ikidai kuwa chombo hicho ni cha kibeberu na kibaguzi.
Haya yanajiri baada ya Baraza la Mawaziri la nchi hiyo kuidhinisha pendekezo la kujiondoa kwenye mkataba huo, lililowasilishwa na chama tawala nchini humo cha SWAPO.
Kadhalika chama hicho cha Rais Hage Geingob kimeiagiza Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya nchi hiyo kuangalia upya sera zake za kigeni ili kutatua masuala yote ya kiufundi yatakayoweza kukwamisha mchakato huo.
Chama hicho kimekuwa kikikariri mara kwa mara kuwa, ICC inatumika vibaya kuwadhalilisha viongozi wa bara Afrika na nchi nyinginezo zinazostawi kiuchumi.
Hii ni katika hali ambayo, Kenya pia imekuwa ikitishia kujiondoa kwenye mkataba huo, kwa kumuandama Naibu wa Rais wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki William Ruto, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kuhusika na machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007, ambapo watu zaidi ya 1,300 waliuawa.
Chanzo:iribuswahili
***************************************************************
26/11/2015 >>> KENYA
Awali katika mkutano na viongozi wa dini mbalimbali, alisema dini haifai kutumiwa kuvuruga akisema “Mungu ni Mungu wa amani.”
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa makanisa mengine akiwemo kiongozi wa Kanisa la Kiangilikana Kenya Dkt Eliud Wabukala.
Viongozi wa dini ya Kiislamu Kenya pia wamehudhuria mkutano huo, wakiongozwa na Prof Abdulghaful El-Busaidy.
Papa Francis amesema amekuwa akihakikisha kila aendako anatangamana na watu wa dini na imani nyingine.
Wakati wa ibada ya misa ambayo ilianza saa nne asubuhi, Papa Francis alisisitiza umuhimu wa familia katika jamii na kupinga utoaji wa mimba.Watu waliohudhuria ibada hiyo walianza kuingia uwanjani mapema na walivumilia mvua ambayo ilianza kunyesha mapema asubuhi.
Chanzo:bbcswahili
************************************************************
MAREKANI
Viongozi wa pande zinazopingana
Sudan, hawajaunda serikali ya mpito katika kipindi cha siku 90 kama
ilivyokubaliwa mwezi wa 8.
Marekani imeonya kwamba mpango huo
wa amani utapata ufumbuzi pale serikali hiyo ya mpito itakapoanzishwa.
Imesema mapigano yamekuwa
yakiendelea kila siku na hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya.
Maelfu ya watu wameuawa tangu Rais
Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar walipovurugana Desemba mwaka 2013.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani
imezitaka pande zote kushiriki mkutano wa kwanza wa pamoja utakaofanyika siku
ya Jumamosi mjini Juba.
Chanzo:bbcswahili
************************************************************
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran IAEO Ali Akbar Salehi amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran yaliyopewa jina la Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA yatakuwa yametekelezwa kikamilifu kufikia Januari 15 mwakani.
Ali Akbar Salehi amesema iwapo mikakati yote itaenda kama ilivyopangwa, basi makubaliano hayo yataanza kutekelezwa kuanzia mwishoni mwa mwezi ujao wa Disemba na kutamatika kufikia Januari 15.
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran ameongeza kuwa, Tehran inaipa kipaumbele sayansi na teknolojia kwa minajili ya kuwepesisha utoaji wa huduma za msingi kwa wananchi.
Kadhalika ameashiria pia ripoti mpya ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, Yukiya Amano na kueleza kuwa ripoti hiyo ni nzuri na imeonesha kwamba Iran imetekeleza ahadi zake na hakuna ukengeukaji wowote katika shughuli zake za amani za nyuklia.
Itakumbukwa kuwa, Julai 14 mwaka huu, Iran na nchi za kundi la 5+1 zilifikia mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama JCPOA. Kwa mujibu wa mapatano hayo yaliyotiwa saini huko Vienna mji mkuu wa Austria, Iran itapunguza baadhi ya shughuli zake za nyuklia mkabala wa kuondolewa vikwazo vya kidhalimu vya kiuchumi dhidi yake.
Chanzo:iribswahili
**********************************************************
26/11/2015 >>> UFARANSA
Rais Francois Hollande wa Ufaransa leo anatarajiwa kuwa na mazungumzo na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kidiplomasia, kupata muungano mpana zaidi katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislamu-IS, baada ya mashambulizi ya mjini Paris Novemba 13, ambapo watu 130 waliuawa.
Kabla ya kuelekea Moscow, Hollande alikutana na Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi mjini Paris asubuhi ya leo.
Rais huyo wa Ufaransa ambaye alikuweko Washington Jumanne, kwa mazungumzo na Rais Barack Obama kuhusu suala hilo, anaelekea kupata uungaji mkono mdogo hadi sasa na kampeni yake imetatanishwa na mzozo wa kibalozi wa hivi karibuni kati ya Urusi na Uturuki.
Uturuki iliidungua ndege ya kivita ya Urusi inayosema ilikuwa imeingia katika anga yake na kupuuza onyo la mara kadhaa. Hata hivyo Urusi imesema ndege hiyo ilikuwa ndani ya Syria ikitekeleza majukumu yake ya kupambana na IS.
Hapo jana (Jumatano) katika mazungumzo na Hollande mjini Paris, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, aliahidi kuiunga mkono Ufaransa katika vita vyake dhidi ya Dola la Kiislamu, na kwamba Ujerumani itatafakari jinsi inavyoweza kusaidia.
Chanzo: dwswahili
************************************************************
26/11/2015 >>>> VENEZUELA
Mwanasiasa wa upinzani nchini Venezuela amepigwa risasi na kuuwawa katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi, kabla ya uchaguzi wa bunge katika muda wa karibu wiki mbili zijazo.
Luis Manuel Dias kutoka chama cha Democratic Action, alikuwa katika mkutano mjini Altagracia katika mkoa wa kati wa Guarico, wakati alipopigwa risasi na watu waliokuwa na silaha ndani ya gari moja .
Katibu mkuu wa chama hicho Henry Ramos ameyashutumu makundi yenye silaha kutoka chama tawala cha United Socialist of Venezuela kwa mauaji hayo.
Taifa hilo la Amerika kusini litakuwa na uchaguzi wa bunge Desemba 6.
chanzi : dwswahili
************************************************************
No comments
Post a Comment