Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » HIZI HAPA KIMATAIFA JIONI YA DEC.11/2015
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Marekan

Afisa mmoja wa polisi mjini Oklahoma amepatikana na hatia ya ubakaji pamoja na kumnyanyasa mwanamke mmoja mweusi katika eneo la umasikini alilokuwa akifanya kazi.

Daniel Holtzclaw mwenye umri wa miaka 29 aliwasimamisha wanawake hao akiwa katika doria za kikazi, kabla ya kuwapekua na baadaye kuanza kuwanyanyasa.

Holtzclaw alipatikana na hatia ya kuwanyanyasa waathiriwa wanane ikiwemo bibi mmoja aliye katika miaka yake ya hamsini pamoja na msichana mmoja wa miaka 17.

Baraza la waamuzi lilipendekeza hukumu ya miaka 263.

Anatarajiwa kuhukumiwa mnamo mwezi Januari.

''Haki imetendeka leo na muhalifu aliyevaa sare anaelekea jela'',wakili wa kaunti ya Oklahoma David Prater alisema.

Hukumu hiyo ilitolewa katika siku ya kuzaliwa ya Holtzclaw,ripota mmoja katika kesi hiyo alituma kanda ya video ya wafuasi wa mwathiriwa katika mtandao wa twitter wakiimba happy birthday baada ya hukumu hiyo kutolewa.

Kesi hiyo imevutia hisia nyingi katika mitandao ya kijamii,huku baadhi ya watumiaji wake wakidai kwamba vyombo vya habari hawakuiangazia.

bbcswahili
**************************************************************************

Burundi

Mashirika ya ndege ya Kenya Airways na RwandAir yamesitisha safari zake za kuelekea mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, kufuatia makabiliano ya risasi mjini humo.

Kwa mujibu wa afisa mkuu wa mawasiliano wa shirika la ndege la Kenya, KQ, Wanjiku Mugo, safari hizo zimesitishwa kutokana na ukosefu wa wafanyakazi katika uwanja wa ndege wa Bujumbura.

Serikali ya Burundi imesema uwanja huo haujafungwa ila tu shughuli zimetatizika kwa sababu wafanyakazi hawakuweza kufika katika uwanja huo, kutokana na makabiliano makali ya risasi kati ya wapinzani wa serikali walioakuwa wamejaribu kuvamia kambi kadhaa za kijeshi mjini humo.

Shirika la kimataifa ya Msalaba mwekundu ICRC nalo kwenye Twitter limesema kuwa halikufanikiwa kuingia katikati mwa mji mkuu Bujumbura kutokana na vizuizi vilivyowekwa na maafisa wa jeshi ambao wanaendelea na msako dhidi ya watu wanaomiliki silaha.

Ripoti zinasema kuwa watu wanane wameuawa kwenye makabiliano hayo huku wengine wengi nao wakiwa wamejeruhiwa.

Mitaa ya Mutakula na Musaga ndiyo iliyoathirika zaidi huku wakaazi wa mitaa hiyo wakirpoti milio ya risasi kuanzia saa kumi alfajiri.

Huku hayo yakijiri Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza ameongoza mkutano wa baraza lake la mawaziri.

Msemaji wa rais Willy Nyamitwe amesema lengo la mkutano huo limekuwa kujadili bajeti ya serikali ya mwaka ujao.

Kuhusu makabiliano ya asubuhi, Bw Nyamitwe amesema kuwa watu wenye silaha walijaribu kuvamia kambi kadhaa za kijeshi, katika kile alichokitaja kama jaribio la kutaka kuwaachilia huru wafungwa.

Nyamitwe amesema kuwa juhudi hizo zimezimwa na Jeshi na kuwa hali ya utulivu imeanza kurejea.

Machafuko yalianza nchini Burundi Aprili mwaka huu, wakati rais Nkurunziza alipotangaza kuwa atawania muhula wa tatu kinyume na mkataba wa Arusha uliosainiwa zaidi ya muongo mmoja uliopita.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa zaidi ya watu 200 wameuawa tangu machafuko hayo kuanza huku maelfu ya wengine nao wakikimbia nchi jirani.

bbcswahili
***********************************************************************

Syria

Kundi la wapiganaji wa Islamic State limejipatia zaidi ya dola milioni 500 kupitia uuzaji wa mafuta kulingana na afisa mmoja wa wizara ya fedha nchini Marekani.

Mteja wake mkubwa amekuwa rais wa Syria Bashar al Assad,licha ya vita vya kutaka kuiangusha serikali.

IS imeiba takriban dola bilioni moja kutoka maeneo inayodhibiti.

Muungano unaoongozwa na Marekani umekuwa ukishambulia maeneo ya kundi hilo ikiwemo maeneo ya mafuta nchini Syria na Iraq kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Afisa anayesimamia fedha katika kundi hilo aliuawa hivi majuzi katika mashambulio hayo kulingana Pentagon.

''Pande hizo mbili zinakabiliana vilivyo lakini pia zinashirikiana katika biashara zinazogharimu mabilioni ya madola'', alisema Szubin kuhusu Syria na IS katika tamko lililotolewa na kituo cha habari cha Reuters.

Kundi hilo limedaiwa kutengeza zaidi dola milioni 40 kwa mwezi kutoka kwa biashara hiyo ya mafuta ikiwemo wanunuzi kutoka Uturuki.

Ukatizaji wa fedha wa kundi hilo ulikuwa miongoni mwa mikakati ya muungano huo kulishinda kundi hilo.

Ikilinganishwa na makundi mengine ya kigaidi ,IS halikutegemea ufadhili kutoka kwa wafadhili wa kigeni bali lilijapatia fedha kutokana na oparesheni zake, alisema Szubin.

Muungano unaoongozwa na Marekani hivi majuzi ulizindua kampeni za kijeshi kwa jina Wave 2,na kuimarisha mashambulio ya angani katika visima vya mafuta vinavyomilikiwa na IS,viwanda vya kusafishia mafuta na magari yanayotumiwa na kundi hilo.

bbcswahili
****************************************************************

Zimbabwe
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka wanasiasa kukoma mara moja kugombania kuhusu nani atamarithi.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 91, amesema hayo katika kongamano la kila mwaka la chama tawala- Zanu-PF huko Victoria Falls.

Pia amevishutumu vikosi vya jeshi, Polisi na idara ya ujasusi kwa kuungana na wanaopigania wadhfa wa urais huku wakijadiliana kuhusu ni nani atakayechukua mahala pake.

Bw Mugabe amesema kuwa hakuna mabadiliko katika uongozi wa taifa hilo.

Waandishi habari wanasema kuwa, kumekuwa na tetesi kuwa mkewe, Grace Mugabe, huenda akapandishwa cheo na kuwa makamu wa Rais.

Bbcswahili

*************************************************************************

Yemen

Shirika la Amnesty International limeilaumu Saudi Arabia na washirika wake kwa kushambulia shule nchini Yemen.

Amnesty inasema kuwa tangu muungano unaoongozwa na Saudi Arabia uanzishe mashambulio ya angani mwezi Machi, zaidi ya shule 20,000 zimeharibiwa huku robo ya shule hizo zikiharibiwa kabisa.

Kwenye ripoti mpya, Amnesty inataka Marekani na Uingereza kusita kuiuzia silaha Saudi Arabia ikisema kuwa silaha hizo zinatumiwa kwa vitendo vinavyokiuka sheria za kimataifa nchini Yemen.
Zaidi ya watu 6000 wanaripotiwa kuuawa katika mzozo nchini Yemen.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / HIZI HAPA KIMATAIFA JIONI YA DEC.11/2015

No comments :