Marekani inasema kuwa mtu mmoja
anayetuhumiwa kuhusika pakubwa katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda
mwaka 1994, amekamatwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Ni mmoja kati ya washukiwa tisa wakuu wanaosakwa na Umoja wa Mataifa.
Wengine wanane bado hawajulikani waliko.
Marekani ilikuwa imeahidi zawadi ya dola 5 milioni kwa atakayesaidia kukamatwa kwake.
Idara ya ulinzi nchini Rwanda imekuwa ikimtuhumu kwa kuwa mchochezi mkuu na mpangaji wa mauaji ya kimbari katika wilaya ya Butare, kusini mwa Rwanda.
No comments
Post a Comment