MAREKAN
Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 20 wameuawa na wengine 120 wamejeruhiwa katika mapigano ya wiki mbili kati ya makundi hasimu ya wabeba silaha katikati mwa Somalia.
Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA)) imesema kuwa, mapigano hayo yaliyoanza Novemba 22 aidha yamesababisha watu zaidi ya 90 elfu kufurushwa kutoka makazi yao.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa, mapigano hayo yalianzia katika mji wa Galkayo, kati ya kundi la wabeba silaha linaloliunga mkono eneo lenye mamlaka ya ndani la Puntland na kundi la waasi linalotoka katika wilaya za Galmudug.
Habari zaidi zinasema kuwa, machafuko yamepungua lakini mapigano hayo yamekuwa yakiendelea licha ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa juma lililopita.
Mji wa Galkayo umekuwa ukishuhudia mapigano ya mara kwa mara kati ya makundi hasimu ya kisiasa na kijamii, mbali na hujuma za mara kwa mara za kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab ambalo linaipiga vita serikali kuu ya Mogadishu.
bbcswahili
*********************************************************************
GHANA
Jaji Mkuu Georgina Theodora Wood amesema uamuzi huo umechukuliwa kufuatia uchunguzi wa kina wa madai ya ufisadi yaliyokuwa yakiwaandama majaji hao.
Kadhalika amesema kuwa majaji wengine 12 wa Mahakama Kuu nchini humo wanaendelea kuchunguzwa kutokana na tuhuma za ufisadi zinazowazonga.
Jaji Mkuu wa Ghana amesema Baraza la Majaji litaendeleza wimbi hilo, ili kuisafisha sura idara ya mahakama ambayo imechafuliwa jina kwa madai ya ulaji rushwa.
Itakumbukwa kuwa, mwezi Agosti mwaka huu, mwandishi wa habari mpekuzi nchini humo anayefahamika kama Sammy Darko, alifichua uozo mkubwa ndani ya idara ya mahakama, katika makala yake iliyoonyesha kuwa baadhi ya majaji wanapokea rushwa ikiwemo ya kuwalazimisha 'wateja wao' kushiriki ngono, ili waathiri maamuzi katika kesi zinazowakabili.
bbcswahili
********************************************************************
Umoja wa mataifa umesema idadi ya wakimbizi wanaotaka kuingia Jordan imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika wiki za hivi karibuni, ikujumuisha watoto kadhaa,watu wazima na wagonjwa.
nchi hiyo imefunga njia zote za panya zinazotoa mwanya wa watu kuingia nchini humo kiholela,takriban miezi nane iliyopita na wakimbizi walio wengi wameondoka nchini humo .
Hata hivyo umoja wa mataifa unakadiria kuwa Jordan bado ina idadi ya wakimbizi wapatao laki sita wa Syria.
kikundi cha kinachoendesha kampeni cha kutetea haki za binaadamu kimeishutumu Jordan kwa kuhatarisha uhai kwa kuzuia wakimbizi wapya kuingia nchini mwake.
bbcswahili
***********************************************************
ETHIOPIA
Zaidi ya raia milioni 10 wengi wao wakiwa watoto wadogo wa Ethiopia
watahitaji msaada wa dharura wa chakula kufikia Januari mwakani.
John Graham, afisa wa shirika la kimataifa la Save the Children amesema zaidi ya Waethiopia milioni 10.1, wakiwemo watoto milioni 6 watahitaji msaada wa chakula kufikia Januari mwaka ujao wa 2016 katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Ethiopia inapitia kipindi kigumu cha kiangazi, kinachohesabiwa kuwa kikubwa zaidi nchini humo katika muda wa miongo mitano, kutokana na athari za hali mbaya ya hewa ya El-nino.
Inakadiriwa kuwa watu milioni 32 watahitaji msaada wa chakula katika eneo la Afrika Mashariki na Kati kufikia mwanzoni mwa mwaka ujao.
iribswahili
********************************************************************
YEMEN
Serikali ya Yemen imesema pande mbili zinazohasimiana zinajiandaa kuanza wiki moja ya usitishwaji mapigano wakati mazungumzo ya amani yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa yakiendelea Uswisi.
Kwa miezi kadhaa sasa Umoja wa mataifa umejaribu kuwaleta pamoja
wanajeshi tiifu kwa serikali ya Yemen na waasi wanaoungwa mkono na Iraq,
ili kumaliza mapigano yaliyosababisha mauaji ya maelfu ya watu na
kulisukuma taifa hilo katika mgogoro wa kibinaadamu.
"Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali na waasi yanapaswa kuanza kutekelezwa kuanzia tarehe 15 Desemba na majadiliano kuanza moja kwa moja," alisema waziri wa mambo ya nje wa Yemen Abdel Malak al-Mekhlafi alipozungumza na shirika la habari la AFP.
"Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali na waasi yanapaswa kuanza kutekelezwa kuanzia tarehe 15 Desemba na majadiliano kuanza moja kwa moja," alisema waziri wa mambo ya nje wa Yemen Abdel Malak al-Mekhlafi alipozungumza na shirika la habari la AFP.
Ould Cheikh ameongeza kuwa wajumbe wa pande tatu watahudhuria mazungumzo hayo yatakayofanyika nje ya mji wa Geneva na kudumu kwa muda ambao bado haujajulikana.
Wajumbe wa pande tatu watahudhuria mazungumzo ya amani Geneva
Mazungumzo hayo yatalenga maeneo manne muhimu, ikiwemo usitishwaji wa kudumu wa mapigano, na kuondolewa makundi yaliojihami katika maeneo wanayoyadhibiti. Mikakati ya kujiamini utakuwa suala jengine litakalojadiliwa ikiwemo kutanua uingiliaji katika maeneo kunakohitajika misaada ya kiutu ambapo wafanyakazi wa kutoa misaada hiyo wameuwawa na kutekwa nyara.
Wajumbe hao watajaribu kutafuta mustakbal wa kisiasa nchini Yemen, taifa lililokumbwa na mgogoro mbaya tangu wapiganaji walipoudhibiti mji mkuu sanaa hatua iliyosababisha serikali kukimbilia Saudi Arabia kabla ya kurejea katika mji wa pili kwa ukubwa wa Aden mwezi uliyopita.
Dwswahili
*****************************************************************************************************
UTURUKI
Vita vya maneno kati ya Uturuki na Urusi vinazidi kushika kasi, baada ya Uturuki kuelezea uwezekano wa kuchukua hatua dhidi ya Urusi na kusema kwamba itaweka vikwazo iwapo itahitajika kufanya hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu wakati akizungumza bungeni na wabunge wa chama chake kinachotawala cha AK. Hata hivyo, ameongeza kusema nchi yake itaendelea kuacha milango wazi kwa ajili ya mazungumzo na Urusi.
Urusi imeweka vikwazo kadhaa vya kiuchumi dhidi ya Uturuki, baada ya Uturuki kuidungua ndege ya kivita ya Urusi karibu na mpaka na Syria na Uturuki, mwezi uliopita, kutokana na Uturuki kudai kuwa ndege hiyo ilipuuza onyo lililotolewa mara kadhaa la ndege hiyo kuvuka mpaka na kuingia katika anga yake.
Hata hivyo, Urusi ambayo imeyakanusha madai hayo, imelijibu shambulizi la Uturuki kwa kupeleka mfumo wa kuweka ulinzi angani kukinga makombora ya masafa marefu katika kambi yake nchini Syria.
Aidha, Davutoglu amesema anataka kuzuru Iraq, haraka iwezekanavyo kujaribu kutuliza mzozo kuhusu hatua ya Uturuki kuwapeleka wanajeshi wake nchini Iraq kuwapatia mafunzo wenzao katika mapambano dhidi ya kundi lenye itikadi kali la Dola la Kiislamu-IS.
''Nimemwandikia barua Waziri Mkuu wa Iraq, Haidar Abadi. Nina matumaini Waziri wa Ulinzi wa Iraq atazuru Uturuki hivi karibuni na mimi nitazuru Baghdad kwa ajili ya mkutano wa ngazi ya juu utakaozungumzia mashauriano. Nataka kuwaeleza watu wa Iraq kwamba siku zote tutawasaidia kupambana na ugaidi. Wairaqi wote ni ndugu zetu,'' alifafanua Davutoglu.
Serikali ya Iraq imesema haijawahi kukialika kikosi kama hicho na italiwasilisha suala hilo katika Umoja wa Mataifa, iwapo hawatoondolewa. Davutoglu amesema zaidi ya watu 2,000 wamepatiwa mafunzo katika kambi hiyo ya kaskazini mwa Iraq.
Dwswahili
***********************************************************************************************************
No comments
Post a Comment