San Bernardino
Watu wawili waliopanga mashambulizi
ya San Bernardino yaliyowauwa watu 14 walifanya mazoezi ya shambulio
hilo siku kadhaa kabla ya kulifanya, shirika la ujasusi la FBI limesema.
Alisema wote walipata mafunzo ya itikadi kali na wamekuwa na itikadi hizo ''kwa muda''
Marekani inachunguza shambulio hilo la wiki iliopita , lililotokea kwenye kituo cha afya , kama kitendo cha ugaidi.
Lakini Bwana Bowdich amesema bado hawajapata ushahidi wowote kwamba mkasa huo wa wiki jana , ambao ni mkubwa wa kigaidi tangu shambulizi la 9/11, ulipangwa nje ya nchi.
Washambuliaji wote wawili waliuawa wakati polisi walipowafyatulia risasi.
bbcswahili
*****************************************************************************
Washington
Mgombea mtarajiwa wa uraisi kupitia
chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump ametaka Waislamu
kuzuiwa kuingia nchini Marekani kwa muda.
Ikulu ya Marekeni imesema tamko la Trump linaenda kinyume na maadili ya taifa la Marekani na maslahi ya usalama wa taifa.
Tamko hilo la Donald Trump limekuja siku chache baada ya watu kumi na nne kuuwawa katika shambulio la risasi zilizopigwa katika mkusanyiko wa watu na wanandoa ambao ni Waislamu.
Shirika la kijasusi la Marekani FBI limesemaSyed Farook na Tashfeen Malik walipandikizwa itikadi kali lakini hawajui na nani na ni kwa namna gani.
Wote wawili waliuwawa na polisi.
FBI walioko California,wameivamia nyumba inayoshukiwa kuhusika katika shambulio hilo na kusema imepata mabomba kumi na tisa ambayo yangeweza kutumika kutengenezea mabomu katika nyumba yao iliyoko Redlands huko California.
Vyombo vya habari vya Marekani vinasema nyumba hiyo ni ya rafiki ambaye anaaminika kuwa alifanya manunuzi ya bunduki zilizotumika katika shambulio
Bbcswahili
****************************************************************************************************
Burundi
Mkutano wa ngazi za juu wa kujadili
hali nchini Burundi utaanza leo mjini Brussels, Ubelgiji mada kuu ikiwa
msukosuko wa kisiasa nchini humo na uhusiano wake na Umoja wa Ulaya.
Umoja wa mataifa umesema kwamba nchi ya Burundi imeshindwa kuheshimu vipengele muhimu katika mkataba wa ushirikiano na kuvitaja vipengele hivyo kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu, kanuni za kidemokrasia na utawala wa sheria na kusema kwamba inaangazia zaidi kuanzisha utaratibu wa kufungua kifungu cha 96 cha mkataba huo wa Cotonou.
Kwa kanuni ya ibara ya 96 ya mkataba wa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya ni kuijengea uwezo nchi ya Burundi ili ichukue hatua katika muda maalum uliowekwa katika maeneo ambayo demokrasia ina walakini, haki za binadamu zinakiukwa na utawala mbovu wa sheria juu ya msingi wa kanuni zilizowekwa katika mkataba wa makubaliano ya mjini Arusha,kinyume na makubaliano hayo ,hatua za kuwekewa vikwazo zitafuata.
Umoja wa ulaya ni mfadhili mkubwa wa Burundi wakati Ubelgiji imeweka makao yake makuu nchini humo na ni nchi ya kwanza baina ya nchi wahisani kwa koloni lake la zamani.
Serikali ya ya Burundi inaandaa bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2016 na nusu ya bajeti yake inategemea misaada ya kigeni.
Katika tukio la hivi karibuni la kurushiana maneno na ubelgiji na umoja wa ulaya ,chama tawala nchini burundi cha CNDD FDD kimesema kwamba nchi hiyo haitahitaji misaada ya kigeni.Baada ya yote hayo chama hicho kikaongeza kwa kusema kwamba asilimilia themanini ya wafadhili inarudi katika nchi za Magharibi.
dwswahili*****************************************************************************************************

****************************************************************************
Marekani
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana na Rais wa Marekani Barack Obama, pamoja na viongozi waandamizi wa seneti na wa wizara ya ulinzi mjini Washington.
Balozi wa Marekani kwenye baraza hilo Samantha Power amesema ziara yao mjini Washington inadhihirisha ukubwa wa kitisho kinachoikabili dunia, na haja ya ushirikiano wa kimataifa kukabiliana na kitisho hicho.
Bi Power aliandaa ziara hiyo jana, ambayo imejumuisha nchi 15 wanachama wa sasa wa Baraza la Usalama, na nchi nyingine tano ambazo zimechaguliwa kujiunga na baraza hilo hivi karibuni.
Ameongeza kuwa Rais Obama na maafisa wengine wa Marekani wametuma ujumbe ule ule, kwamba dunia inapaswa kushirikiana katika kutatua migogoro iliyopo wakati huu, kuanzia kitisho kundi la itikadi kali za Dola la Kiislamu, na mizozo mingine ikiwemo wa Syria, Burundi, Sudan Kusini na Yemen.
dwswahili
******************************************************************************************************
No comments
Post a Comment