Klabu
ya Barcelona ya nchini Hispania imefanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa
na wapinzani wao wakubwa Real Madrid ambayo waliiweka mwaka 2014.
Real
Madrid mwaka jana ilifanikiwa kufunga magoli 178 ambayo yalikuwa
hayajawahi kufungwa na klabu yoyote katika historia ya klabu ya
Hispania.
Awali
kabla ya mchezo kati ya Barcelona na Real Betis, Barcelona ilikuwa na
magoli 176 na baada ya kuibuka na ushindi wa goli nne kwa bila dhidi ya
Real Betis sasa Barcelona ndiyo timu inayoongoza kwa kufunga magoli
mengi kwa mwaka mmoja kwa kuwa na magoli 180 na kuiacha Real Madrid
ikiwa na magoli 178.
Kati
ya magoli 180, Lionel Messi amefunga magoli 48, Suarez 48 na Neymar 41
ambayo ni sawa na asilimia 75 ya magoli yote ambayo Barcelona imefunga.
Aidha katika mchezo huo, mchezaji bora wa dunia mara nne, Lionel Messi alifanikiwa kufikisha michezo 500 akiichezea Barcelona.
TAZAMA HIGHLIGHTS ZA MAGOLI YOTE HAPA>>>>>>>>>>>
No comments
Post a Comment