Wastara ni Mwigizaji wa Bongo Movie, kulikuwa na picha chache zikizunguka mitandaoni zikimwonesha Wastara akifunga ndoa mtu aliyetajwa kuwa ni Mbunge, ninazo picha pamoja na maneno yake akithibitisha nda yake mpya.
Wastara kapost picha kwenye account ya Instagram na kuandika haya >>’Nilikuwa kwenye usingizi mzito nimeshtuka nikakumbuka ni vizuri kuwapa asante wale wote walipiga goti kuniombea siku moja nipate faraja au tulizo la moyo ama stara kwa mwanamke wa kiislam kama dini inavyosema.. Japo kwangu nilikuwa nimeweka nadhiri ya miaka 3 ikipita basi ridhki ya mume ikija milango iko wazi alhamdulilah imekuja wakati muafaka na siku muafaka baada nadhiri yangu kutimia. Mungu ni mwema sana namuamini sana na ananipenda sana ndio maana kaniumba anavyojua yeye tumshukuru mungu kwa hili, najiombea na wale wenye nia njema na mim tuwe pamoja, iwe yenye neema ndoa hii aliyoipanga mungu pekee yeye ndie mwenye mamlaka juu ya hili barka, rehma, stara, uvumilivu ridhiki, upendo uwe juu yetu na bi mkubwa niliyemkuta aliyenipokea kwa mikono miwili kama mke mwenziwe msiumize vichwa tunajuana tunaheshimiana.’- @wastara84
Hizi ni baadhi ya picha zake nyingine alipost Wastara kwenye tukio zima la ndoa yake.
No comments
Post a Comment