Mgombea wa urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia
wananchi kwenye kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa
Jamhuri mjini Dodoma leo akiendelea na kampeni zake za kuisaka Ikulu
nchini Kote akiwaomba watanzania kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba
25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ili aweze
kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.
Akitoa hotuba yake katika moja ya
mikutano yake alioufanya katika mji wa Kibaigwa Dk. John Pombe
Magufuli amesema hakuna kitu kinachomuumiza kama mauaji ya wakulima na
wafugaji tanayotokea kati ya wilaya za Kongwa Mkoani Dodoma na Kiteto
mkoani Manyara ni jambo ambalo linamuumiza sana kwani watanzania
tumezoea amani na si mapigano.
Ameongeza kwamba katika serikali
yake mara baada ya kuchaguliwa na kuunda serikali ni jambo ambalo
ataliangalia kwa umiakini mkubwa.
“Yaani Mimi Magufuli Nimteuwe Waziri
na watendaji wengine wa serikali alafu Mauaji yatokee watu wafe.
Mkuu wa
mkoa yupo , Mkuu wa wilaya yupo na Kamanda wa Polisi yupo wabaki
wanapunga upepo, wamiliki wa Ng’ombe wabaki wanakula maisha haiwezekani
Nitalala nao mbele na Ng’ombe wataliwa msibani kwa uzembe
waliosababisha”
Magufuli amewataka wafugaji na
wakulima kuishi kwa amani bila kubaguana lakini pia akasema atatumia
sheria za ardhi na kuhakikisha maeneo ya wafugaji na wakulima
yanatengwa, ili wafanye shughuli zao na kukuza kipato na uchumi wao
bila kusumbuliwa.
No comments
Post a Comment