Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu mtandao wa Twitter kuongeza idadi ya maneno ya kutweet kwa Tweet moja… kwa sasa Twitter inamruhusu mtumiaji kutumia uwingi wa maneno 140 tu kutweet message moja lakini kwa wale ambao wanapenda kuchat kwa marefu, Twitter iliamua kongeza idadi ya maneno kufikia 10,000 kwa private messages.
Nimekutana na habari muda huu ambayo ningependa kushare na wewe mtu wangu… inasemekana kuwa Twitter ipo kwenye mpango wa kuongeza idadi ya maneno ambayo mtu anaweza kuandika kwa Tweet moja na kwa mujibu wa mtandao wa http://www.complex.com Twitter ina mpango wakuleta huduma itakayowaruhusu watumiaji wake kutweet ama kuandika Tweets/post zenye maneno zaidi ya 140!
Baadhi ya mitandao kama Re/Code wa Marekani wanaamini kuwa maamuzi haya yamesukumwa na mabadiliko ya idadi ya maneno ya kutumia kwenye private messages za Twitter… >>> “watu
wamepokea vizuri ongezeko la maneno ya Twitter kwenye message za
private, hii inaonyesha jinsi gani ambavyo bado kampuni ina nafasi ya
kukua zaidi ya hapa…” <<< mmoja ya wafanyakazi wa Twitter aliuambia mtandao wa Re/Code.
Je Twitter itaweza
kukuza biashara yake katika ushindani wa Teknolojia na mitandao ya
kijamii safari hii? Kama ilikuwa haijakufikia basi ichukue hiyo mtu
wangu na pengine tutegemee kufaidika very soon na mpango huu!
No comments
Post a Comment