Na John Banda, Dodoma
MTU mmoja mkazi wa Kizota Manispaa ya Dodoma amejinyonga mpaka kufa Baada ya Kudhani amemuua mama yake mzazi kwa kumchoma visu mara 3 katika maeneo ya Tumboni, shingoni na ubavuni siku ya Christmas.
Katika taarifa iliyotumwa na jeshi la polisi kwa vyombo vya habari ilionyesha kuwa Des,25 mwaka huu majira saa 12:00 jioni huko Kizota Mbuyuni Manispaa ya Dodoma, mtu mmoja aitwaye TATU OMARI, miaka 74 alijeruhiwa kwa kuchomwa na kisu tumboni, shingoni na ubavuni na mtoto wake aitwaye HAMISI ISSA, miaka 40.
Taaarifa Imesema mara baada ya tukio hilo Issa alijifungia chumbani kwake na kujinyonga hadi kufa akidhani amemuua mama yake huku ikibainisha kuwa Chanzo chake ni ulevi wa pombe kupindukia.
Taarifa hiyo ilisema Matukio mengine yaliyojiri katika kipindi cha sikukuu watu watatu wamekamatwa kwa makosa ya kupatikana na Bhangi kinyume cha sheria ambapo SOPHIA PAUL [16], mkazi wa eneo la Itega Manispaa ya Dodoma alikamatwa akiwa na misokoto 47 ya bhangi, REGINADO MARIKI, miaka [27], mkazi wa kijiji cha Mpinga Wilaya ya Bahi alikamatwa na mabunda 23 ya Bhangi MUSSA AUGUSTIN MUHOGO alikamatwa akiwa na Bhangi misokoto 21.
Aidha EXAVERY JONAS MOGOPE, mia [23], mkazi wa Chazungwa Mpwapwa akiwa na sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo ni Kofia aina ya pama, suruali na shati kombati kinyume cha sheria, sare alizoiba baada ya kutoroka mafunzo RUVU JKT mwaka 2013. Watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani jana.
"Natoa shukrani kwa Wananchi wote Wakazi wa Dodoma kwa kutambua kwamba usalama unaanzia majumbani mwao na kusherehekea sikukuu za Maulid na Christimass kwa Amani na utulivu. Ninatoa wito waendeleze utamaduni huo katika kipindi cha sherehe za kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya 2016".
pia nukuu ya imeongeza kuwa "Pia watambue watakaoshindwa kutii sheria bila shuruti wakamatwe na kufikishwa makamani".
No comments
Post a Comment