JINA LA MTO
|
UNAPOPATIKANA
|
UREFU
|
||||
|
Africa
|
|
||||
|
South America
|
6,400 km (3,976
miles)
|
||||
|
Asia (China)
|
6,300 km (3,915
miles)
|
||||
|
America kaskazin {USA}
|
|
||||
|
Europe/Asia (Russia/Mongolia]
|
5,539 km (3,441
miles)
|
Chanzo cha mto ni mahali ambako mto husika unaanza. Mara nyingi ni chemchemi yaani mahali ambako maji yaliyokusanyika chini ya ardhi yanatoka nje na kuonekana kwenye uso wa ardhi. Kwa mito mingine inaweza kuwa mahali ambako mito miwili inaungana na watu wameamua kupatazama kama mto mpya unaanza hasa kama mito asilia haina tofauti sana katika ukubwa wao kwa hiyo haiwezekani kusema mto mmoja unaingia katika mto mwingine. utakuwa unaifahamu mito mingi sana ulimwenguni kwa maumbo na kimo chake, lakini kwa taarifa yako mto mrefu kuliko yote duniani ni mto kutoka Afrika { Afrika Kaskazini} unatokea nchini Misri unaitwa Mto Nile. nimekuwekea Orodha ya mito mitano mirefu zaidi duniani itazame hapa katika muonekano wake pichazzzzzzzz!!! | |||||||
Mto Nile MTO NILE Mto wa Nile hujulikana pia kama Naili; kwa kiarabu { an-nīl) ni mto mkubwa upande wa mashariki ya bara la Afrika. Mara nyingi hutajwa kuwa pia mto mrefu kabisa duniani kushinda mto Amazon . Kutoka Ziwa la Viktoria Nyanza hadi mdomo wake kwenye Bahari ya Mediteranea Nile inahuusiano na nchi za Uganda, Sudan Kusini, Sudan na Misri kwa urefu wa km 6,650. Beseni ya Nile hukusanya maji ya eneo linalojumlisha 10% za eneo la Afrika yote au km² 3,349,000. Takriban watu milioni 250 hukalia beseni hiyo. unadhani maji yake yana matumizi gani kwa afrika? matumizi ni mengi hata kwa baadhi ya jamaa zangu wa kule kagera kikubwa tujivunie yetu. AMAZON RIVER Unapozungumzia mto Amazon unakuwa unazungumzia mto wa pili kwa urefu duniani kwa urefu wa takribani kilomita 6,400. mlima huu unapatikana katika bara la Amerika kusini, lakini kuhusu urefu hakuna mapatano bado kama Nile au Amazonas ni mto mrefu duniani. Makadirio hutegemea ni tawimto upi mwenye chanzo cha mbali zaidi unaokubaliwa na wataalamu. 1969 urefu wake ulipimwa kuwa 6.400 km. Amazonas ina tawimito zaidi ya 10,000 na kati ya hizi kuna 17 zenye urefu wa zaidi ya 1,600 km zikishinda mito kama Senegal, Gambia au Nile ya buluu. Upana wa mto ni wa kilomita kadhaa kufika hadi 100 km wakati wa mafuriko ya kila mwaka. Delta ya Amazonas ina upana wa mamia ya kilomita; ndani yake kuna kisiwa cha Marajó chenye eneo la 49,000 km² ambalo ni kubwa kushinda nchi kama Rwanda au Burundi. mto huu kwa kireno hujulikana kama Rio Amazonas MTO YANGTZE Mto Yangtze pia hujulikana kama Changjiang) ni mto mkubwa nchini China na pia mto mrefu wa Asia yote. Duniani huhesabiwa kama mto mrefu wa tatu baada ya Amazon na Mto Nile). Urefu wake ni kilomita 6,300 nauko ndani ya China. Chanzo chake kiko katika nyanda za juu za Tibet. Inafuata mwelekeo wa kusini-mashariki hadi kilomita 1,500 baada ya chanzo. Kuna miji mingi mikubwa inayotegemea mto huu na machafuko kutoka ya viwanda vyao yamekuwa tatizo. Katika historia mto Yangtze ulikuwa mpaka kati ya China ya kaskazini na China ya kusini. |
Mto Mississippi ni mto mkubwa wa unapatikana marekani na ni mto mkubwa nchini humo pia ni kati ya mito mirefu duniani ukishika nafasi ya nne nyuma ya Mto Nile,Amazonas na mto Yangtze.
mto huu chanzo chake kipo kaskazini mwa Marekani kwenye ziwa Itasca katika jimbo la minnesota. unapitaa katika majimbo ya majimbo ya minnesota,wisconsin,Iowa,Illinois,Missouri,Kentucky,Tennessee,Arkansas,Mississippi,Louisiana na kuishia katika Ghuba ya Mexico karibu na mji wa New Orleans
Mto huu wenye urefu wa kilomita zipatazo 5,539 unapatikana huko Mongoria na ni mto mkubwa zaidi eneo hilo na maji yake unayamwaga katika ziwa Baikal
huu ndio mto ulioshika namba tano katika orodha ya mito mitano mikubwa zaidi duniani katika rekodi za ulimwengu hu.
Kwa msaada wa mtandao nimeweza kukuletea hii .....mwandaaji wako ni Denice John Kazenzele.
enjoy na kazenzele1.blogspot.com
No comments
Post a Comment