picha na maktaba |
Na Peter Mkwavila, Chamwino
WANANCHI katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma wametakiwa kufuata kanuni za afya ili kuondokana na ugonjwa wa kipindupindu ambapo mpaka sasa kuna wagonjwa 125 na vifo vitano.
Mkuu wa Wilaya hiyo Farida Mgomi alisema kulingana na hali hiyo sasa ni marufuku kupika pombe kwenye minada na uzaji wa vyakula.
Pia aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanakuwa na vyoo na kuvitumia ili kuopndoa maambukizi mapya ya ugonjwa huo.
"Tuhamasishane wananchi kufanya usafi kila siku ili ugonjwa huo uweze kutoweka ndani ya wilaya ya Chamwino" alisema
Alitaka usafi wa mazingira uendelee kila kijiji iukiwemo na kufanyika msako wa kubaini wote wanaokiuka masharti na kakuni za afya.
Pia alitaka viongozi wa vijiji kushirikiana na mgambo ili kuwabaini watu wanaouza pombe maporini ili waweze kuchukuliwa hatua.
Akizungumzia juu ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), aliwataka watendaji kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo kwani ni mkombozi wao katika kupata matibabu kwa njia rahisi.
Aliwataka kuondokana na dhana kuwa mfuko huo ni maalum kwa ajili ya watumishi wa serikali lakini upo hata kwa wakulima na wafugaji.
"Inasikitisha baadhi ya maeneo ya vijiji watu wanashindwa kujiunga kwa kisingiziop kuwa hawana fedha lakini watu hao hao wana mifugo wanaweza kuuza na kisha familia nzima kujiunga na mfuko huo ambao unawapa uhakika wa matibabu mwaka mzima" alisema
mwisho
No comments
Post a Comment