Raia wa
Uganda wanapiga kura hii leo ili kumchagua rais atakayeiongoza nchi hiyo, huku nauli
za vyombo vya usafiri zikipandishwa kutokana na raia wengi wakisafiri kwenda
katika maeneo yao ya kupigia kura.
Kutoka nchini Uganda taarifa zinasema kuna kadhia na usafiri
zinazowafanya raia wan chi hiyo wanaosafiri kuelekea maeneo mengine hasa
vijijini kupata taabu.
Hata hivyo polisi wamewataka wananchi kuwa na imani na tume
pamoja na maafisa usalama pia kutoa maelekezo ya kurejea katika shughuli zao
mara baada ya kupiga kura na sio kubaki maeneo ya kupigia kura kwa madai ya
kusubiri matokeo.
Hata hivyo taarifa za hivi punde zimesema kuwa mamlaka ya
mawasiliano nchini humo imekata mawasiliano yote ya mitandao ya kijamii ikiwemo
Facebook,Tweeter,Watsapp,instagram pamoja na njia zote za kutuma na kupokea
fedha kwa njia ya mtandao.
katika ngazi ya urais macho na masikio ya wengi ni kwa Rais
wa sasa Yoweri museven kutoka chama tawala cha NRM, Amama Mbabazi aliyekuwa
waziri mkuu wa rais museven ambaye ni mgombea huru pamoja na mpinzani mkuu wa
rais museven kizza Besigye kutoka chama cha upinzani cha FDC.
hivi sasa Wapiga kura nchini humo
wanaendelea kupiga kura vituoni kuwachagua viongozi, ingawa katika
baadhi ya vituo upigaji kura ulichelewa kuanza.
Mjini Kampala, ambapo makao makuu ya Tume ya Uchaguzi yapo, bado kuna vituo ambavyo kufikia saa nne upigaji kura haukuwa umeanza.
Hata hivyo, tume hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, imeandika: "Tunabaki kuwa na matumaini na tunawahikishia kwamba nyote mtaweza kupiga kura leo. Tunasikitika kutokana na kuchelewa huku. Asanteni.”
Kuhusu iwapo muda wa kupiga kura utaongezwa, tume hiyo kupitia mitandao ya kijamii imesema kwa mujibu wa sheria, ni sharti vituo vifungwe saa kumi alasiri.
Kuna wagombea saba wa urais wanaojaribu kuhitimisha uongozi wa Rais Yoweri Museveni ambaye ameongoza kwa miaka 30 sasa.
Wanaotoa ushindani mkubwa kwa Bw Museveni ni mgombea wa FDC Kizza Besigye na waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi.
Kuna jumla ya wapiga kura 15 milioni ambao wamejisajili kupiga kura nchini humo kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi.
No comments
Post a Comment