Waziri mkuu Kasimu Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Tanga.
Akiwa bandarini hapo waziri Mkuu amehoji kununuliwa kwa matishari matatu yenye uwezo mdogo wakati serikali ilitoa zaidi ya dola milioni kumi kununua matishari mawili ya kisasa.
Kufuatia hali hiyo waziri Majaliwa ameutaka uongozi wa bandari ya Tanga kuandika barua yenye maelezo ya kina itakayokuwa imeweka bayana walioshiriki kwenye ununuzi wa matishari hayo.
Katika ziara hiyo waziri majaliwa alihoji sababu za kununuliwa matishari matatu yenye uwezo mdogo wakati serilali ilitoa dola milion 10.113 kwa ajili ya matishari mawili ya kisasa.
Kufuatia mahojiano hayo Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Hendri Arika alisema hakuwepo wakati wa ununuzi wa vifaa hivyo lakini akamtaka mhandisi wa bandahi hiyo kulitolea ufafanuzi jambo hilo.
Waziri mkuu pia alimuagizaa mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza kukabiliana na uingizwaji wa sukari kupitia bandari bubu ambayo unaikosesha serikali mapato na uzalishaji wa ndani.
No comments
Post a Comment