Aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa
Cuba Fidel Castro amevunja kimya chake kuhusu ziara ya hivi majuzi ya
Rais wa Marekani Barack Obama nchini humo.
Fidel, aliyemkabidhi kakake Raul uongozi wa taifa hilo mwongo mmoja uliopita, amesema Cuba haihitaji zawadi zozote kutoka kwa Marekani.
Akijibu pendekezo la Bw Obama kwamba wakati umefika wa kuunda urafiki na kuzika kwenye kaburi la sahau masalio ya Vita Baridi bara Amerika, Fidel Castro amewakumbusha wasomaji kuhusu uvamizi wa Bay of Pigs uliofanywa na wakimbizi wa Cuba wakisaidiwa na Marekani mwaka 1961.
Amesema maneno ya Obama ya kuhimiza maridhiano ni sawa na “rojo ya sukari” na kuonya kwamba raia wa Cuba wanaweza kupata “mshtuko wa moyo”.
Fidel Castro, 89, aliongoza Cuba kuanzia 1959 hadi 2008 alipomkabidhi nduguye madaraka.
No comments
Post a Comment