Sakata
la Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano),
January Makamba na Mdogo wake Mwamvita kudaiwa kupokea rushwa kutoka kwa
raia wa Italia, Vincenzo Cozzolino ili wamsaidie kupata zabuni ya
ujenzi limechukua sura mpya.
Sauti na jumbe mbalimbali zilizosambazwa na kuwekwa kwenye mtandao na mtu maarufu kwenye mitandao ya kijamii na mmiliki wa tovuti ya U-Turn, Mange Kimambi, raia wa Tanzania aishie Marekani, zinaonesha mazungumzo kati ya watatu hao, mwaka 2011. Jana, Mwamvita na Makamba walikiri kuwa sauti hizo ni za kweli.
Muitaliano
huyo ambaye anadaiwa kumpa Mange Kimambe ushahidi wote wa mawasiliano
kati yake na Ndugu hao, amejitokeza na kuwasafisha akidai kuwa hakuwahi
kuwapa rushwa wala kuhusiana na January kibiashara.
Cozzolino
ameandika ujumbe akidai kuwa ingawa yeye na Mwamvita walikuwa na
uhusiano wa mapenzi mwaka 2011 na baadae kujiingiza katika biashara
binafsi ambayo ilipelekea kugombana kwao, hawakumhusisha January kwa
aina yoyote katika biashara yao.
“Sikuwahi
kumuomba [January] kunisaidia katika biashara zangu. Sikuwahi kumpa
fedha. Mara chache nilizokutana naye ilikuwa ni mazungumzo ya kawaida ya
kijamii. Nilikuwa na uhusiano na Mwamvita. Uhusiano wetu ulikuwa bomba
mwanzoni lakini ukawa na mwisho mbaya,” ameandika Cozzolino.
Awali,
sauti ya January na mwandishi wa habari iliyosambazwa, January
anasikika akieleza kuwa aliwahi kukutana mara moja Dubai na Muitaliano
huyo na kwamba alitambulishwa kama mpenzi wa dada yake.
Alisema
baadae dada yake alimwambia wameanza kufanya biashara ya kahawa na
Muitaliano huyo na baadae biashara hiyo kufa huku ikiwaacha katika
mzozo.
Kwa
mujibu wa Kamamba, Muitaliano aliyekuwa ameweka nusu ya mtaji ambayo ni
dola milioni 50, alianza kudai kiasi hicho cha fedha na sio
vinginevyo.
Alisema
kuwa awali, muitaliano huyo alikuwa anajaribu kumshawishi Mwamvita
amkutanishe na viongozi wakubwa wa serikali ikiwa ni pamoja na Katibu
Mkuu.
Hata
hivyo, Mange Kimambe ambaye ndiye anayeeleza kuwa na nyaraka zote za
ushahidi aliokabidhiwa na Muitaliano huyo na kwamba hivi sasa Muitaliano
amelipwa na kukubaliana kumsafisha Mbunge huyo wa Bumbuli.
Mange
amesisitiza kuwa ana ushahidi wote wa January na dada yake kupokea
rushwa kutoka kwa mfanyabiashara huyo na yuko tayari kuwakabidhi
Takukuru.
Imeandikwa hivi moja ya nakala zilizoonekana.,,,
Yes it is indeed the biggest punishment ever. .
.
Jamani sina ushirikiano wa Muitaliano anymore Ila Muitaliano alishanipa
enough to take them down anyways. .
.
Niko tayari kuwapa Takukuru email hii nzima waone Enzo alichomwandikia
Mwamvita kuhusu January Makamba na kumtishia kuanika! Mpaka Mwamvita
amjibu Hivi......In short it's about January Accepting a huge amount of
cash from Avery questionable character
.
.
Sito publish hapa sabbau pia nitakuwa nawasidia wao ku over their
tracks. Hata Kama wahusika wakidelete hizi email , serikali still ina
uwezo wa kuomba records zooote za email hawa hawa wahusika wooooote. Hii
email Ndo jamaa alikuwa anawatishia cha mwisho mwisho wampe pesa zake
kabla hajaanika issue wakadhani anatania! Kesho yake ndo akaja kwangu.
.
.
Ila dah binadamu wabaya sana, hamuwezi mkaamini mnajua Muitaliano Sasa
Hivi eti ananiomba niache kuposti? Ananiambia niachane na issue And
respect his decision. Imagine, now ananiomba niwaprotect Makambas
especially January. Ananiambia kabisa leave January alone
😂😂😂😂😂😂... Yani ukisoma messages zake wakati kadhulimiwa alivyokuwa
anatia huruma and now unaweza shangaa.. Eti just stop Na huna ruhusa
ya ku publish vitu nilivyokutumia in private . Ila nime mjibu vizuri
nime mwambia I'm glad nimekusaidia Sasa niache niwasaidie Watanzania. I
swear next time kabla sijamsaidia Mtu nitawasainisha mikataba mpaka!
But nilichoelewa Ni kwamba I think kawaambia Kuwa hakuna vitu vingine
alivyonitumia Au alivyoniambia so Sasa wanavurugana.
.
.
You guys know what? Hata Kama serikali ikiangalia pembeni but guess what
2025 is not far tunasubiria CCM watuambie eti January Makamba ndo
mgombea wao waone Kama hatutompa nchi Halima Mdee!! 😂😂😂😂😂😂.
.
.
Oh yeah just to add, ile Safari ya Dubai, hata Mwamvita pia alikuwepo.
In short it's a family affair. Ja Ja Ja Ja....
.
.
Basi immediately baada ya kumalizana Na Muitaliano Mwamvita akaenda
kuweka caption eti NEXT?
No comments
Post a Comment