NENO tumbua jipu ni
kauli mbiu kama zilivyowahi kuibuka nyingine wakati chaguzi mbalimbali
zikiendelea au hata baada ya chaguzi hizo, lakini neon hili limeongezeka zaidi
pengine ni kutokana na uelewa wa wananchi wengi juu ya siasa kwa hivi sasa,
lakini pia labda ni kutokana na wagombea waliosimama kuwania nafasi ya Urais
hasa katika vyama vya CCM na Muungano wa umoja wa katiba ya wananchi {UKAWA}.
Kwa tafsiri sahihi
kutoka katika mkusanyiko wa maana mbalimbali neno “JIPU” au furuncles kwa lugha ya wenzetu Ni maambukizi ya kina ya folikuliti au maambukizi ya
foilikoli za nywele mara kwa mara unasababishwa na maambukizo ya kibakteria
Stafilokokasi aureasi , ambayo husababisha kuvimba kwa eneo chungu lililo juu
ya ngozi kutokana na mkusanyiko wa usaha na tishu mfu.
Lakini
kwa tafsiri ya sasa unapozungumzia neno “jipu” unazungumzia mtu au kiongozi
mwenye mwenendo mbaya katika jamii anayoishi au kuitumikia kama ni kiongozi na neno hili limeibuka mwaka 2015 katika kampeni za aliyekuwa waziri wa ujenzi ambaye
kwa sasa ndiye Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Joseph Pombe
Magufuli wakati wa kampeni kipindi hicho akipiga pushap shana majukwaan, yote
hiyo ilikuwa ni kama sanaa iliyowateka watanzania na kumwamini na kumpatia
ridhaa ya kuliongoza taifa hili.
Hadi
sasa neno jipu limekuwa na kuonekana wazi kufanya kazi baada ya Mh.Rais yeye
mwenyewe kuwatumbua wote walioonekana kubeba jina jipu kwa kuwaondoa katika
nafasi zao katika sekta na wizara mbali mbali kwani tumeona TRA,TAKUKURU,
Mamlaka ya Bandari na kwingineko, lakini pia wapo viongozi wa chini yake
waliofanya kazi hizo wakiwemo Dr Hamis Kigwangala,Mh.Simbachawene,Mh.Seleman
Jafo,Paul Makonda na wengineo dhidi ya ubadhilifu wa mali ya umma na kuhusika
na kashfa mbalimbali lakini pia usimsahau mzee wa kushtukiza Mh Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Katika
kasi hii wengi wanafurahi na kuona kuwa pengine kura zao hazikuharibika kwani
walichokihitaji wanakiona sasa kinatekelezeka, lakini kwangu mimi licha ya
kuona hayo bado nina swali, “ ikiwa unafurahi kutumbuliwa kwa mtu Fulani kwa
kuwa alizuia au alikukosesha haki yako uliyodhani ni yako, wewe vipi unafanya
majukumu yako?” jibu si lazima unipe zaidi ya kulitafakari na kubadilika iwapo
utagundua jipu hilo unalo maana jipu huwa nalo yeyote Yule ilimradi ukipat avimelea vya majipu au maambukizi ya
kina ya folikuliti kwa hiyo nawe pia unaweza kuwa ni jipu umejichunguza?
Yapo
majipu mengi katika jamii kwa mfano nitakupa majipu machache {tabia mbaya kwa
wananchi ambapo hutendeka majumbani mwa wengi} kasha ukijipima mtafute daktari
wa kukusaidia kutumbua maana wewe huna uwezo wa kujitumbua.
A}wizi
– kazi ni kazi kama haina hasara na mikosi!!! Ukikutana na kauli hiyo
utaitafsiri kwa njia tofauti, kwani ukimaanisha ilivyo tamkwa utasema hata wizi
ni kazi lakini sio sawa kwani wizi ni jipu kutokana na kuwadhulumu haki walio
na haki ya kuwa na hicho unachokichukua pasi na ruhusa ya kufanya hivyo, hivyo
unaweza kumkuta mtu anamsema Meneja Fulani katumbuliwa jipu na kudai kuwa
alishawashinda wakati yeye siku moj aau mbili zilizopita kaiibia ofisi yake au
kawaibia watu anaoishi nao kasha anasema ofisa Yule alistahili kutumbuliwa
kwani alitutesa na kutusababishia umaskini..wewe pia ni jipu na anayepaswa
kukutumbua ni Yule anayekuona.
B}masengenyo-
ahahahaha! Binadamu bwana! Kuna tabia mbaya zaidi katika jamii inayowatesa walio
wengi, hii ni tabia ya wivu, wivu una hasara yake katika jamii ya wanadamu.
Wivu
husababisha umaskini, wivu pia husababisha migongano{migogoro} katika jamii,
wivu husababisha kusengenyana, wivu huleta imani za kishirikina, wivu huleta
mauaji na matatizo mengine kama hayo na zaidi ya hayo.
Wivu
ni jipu kuanzia majumbani kwenda maofisini, katika maeneo ya biashara na
kadhalika na palipo na masengenyo daima hakuna maendeleo na pasipokuwepo na
maendeleo kwa sababu ya masengenyo hakika hilo nalo ni Jipu na mimi naweza
kukuonesha anaepaswa kukutumbua wewe ni jipu.
C}uvivu/uzembe-“kufanya
kazi sio kazi na ukiona kazi kufanya kazi basi acha kazi uone ilivyo kazi
kupata kazi” Naupenda sana huu msemo lakini pia unanikumbusha kuwa wapo wat
wali na kazi ambao wanajihisi kuwa ni muhimu kuliko wengine na endapo
wataondoka basi ofisi hiyo itakufa nay eye ana uhakika wa kupata kazi katika
ofisi nyingine kutokana na umaarufu au uwezo wake anaojiamini nao, lakini
kumbuka ukipoteza kazi usahau kupata kazi maana katika ofisi zote unazodhani
kuomba kazi wapo wenye nafasi zao na wanafanya kazi vema, lakini ukiwa mvivu
jua wewe unadhoofisha maendeleo ya nchi na jamii yake, wewe ni Jipu na ukiona
wewe ni mzembe pia jua unahatarisha kutokufanyika kazi za ofisi au eneo husika
au utaharibu sifa ya kazi unayoifanya au kuharibu kabisa sifa ya ofisi hivyo
kwanini tusikuite jipu? Wewe ni jipu, hivyo hakuna haja ya kumwita mwenzako
jipu angali ukijua pia wewe ni jipu kutokana na uvivu au uzembe wako..kwanini
usitumbuliwe?
E}uzinzi”kuna
utofauti kati ya uzinzi na uasherati” Lakini sina sababu ya kukuelezea utofauti
wake lakini kumbuka tu yote yanahusiana na kushiriki tendo la ndoa nje ya ndoa
kama umeoa/kuolewa au kushiriki mapenzi katika wakati ambao hujaruhusiwa
kisheria kufanya hivyo. Na kumbuka hiyo ni dhambi hata maandiko matakatifu
yanatuambia '' Maana Haya Ndiyo Mapenzi Ya MUNGU, Kutakaswa
Kwenu, Mwepukane Na Uasherati- 1 Thesalonike 4:3.'' Tunaamini kuwa hakuna aliye
msafi kama pia biblia isemavyo kuwa 1 Kor 5:10-11'' Sisemi msichangamane kabisa na
wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye
kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. Lakini, mambo
yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni
mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi;
mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.'' Hili nalo ni jipu na hatuna budi kulitumbua
ili kupunguza kasi ya umaskini unaosababishwa na magonjwa na vifo vya vijana
ambao ni taifa la kesho.
G}ulevi-“unapozungumzia
ulevi hatumaanishi pombe pekee, hapa tunazungumzia mambo mbalimbali maana neno
ulevi lina maana ya kuwa na matumizi ya kitu Fulani kupit akiasi
kinachohitajika, kwa mfano wanaotumia pombe, akinywa alafu asilewe akawa
anajitambua haanguzi au hatukani mtu au haongei maneno ya “kipuuzi” bali akiwa
na akili zake timamu huyo tunamuita mnywaji sawa na mnywaji wa maji au
Sharubati {maji}, lakini wapo walevi wa maji, madawa ya kulevya , ngono,n.k nao
hao ni majipu ambayo yanapaswa kutumbuliwa na jamii hapa hatuhitaji nguvu ya
serikali bali ya umma.
H}usaliti-kuna
watu pasipo kuwa na nyumba ndogo hawana raha, wanajiona sio wanaume
waliokamilika, pia wapo wasipokuwa na wanaume nje ya ndoa wanajihisi kuugua
ugonjwa unaofanana na maralia au “TB”, hili nalo ni jipu kwani pasipo kujua
kuna madhara ya kuwa na wanawake au wanaume wa nje kwani uharibu familia
kiuchumi pamoja na kuingiza maradhi katika familia au kwa mpenzi uliyenaye
kwani ukiachana na walio katika familia pia wasaliti wapo hata katika hatua ya
uchumba au katika mapenzi yasiyo rasmi”Girl friends & Boyfriends” ni hatari
kwani baada ya muda kizazi kilichokisiwa kuwa cha baadae hupotelea
kusikojulikana na huku nyuma kuacha majonzi.
Sisemi
kuwa kila mtu ni jipu lakini kwa kuwa hakuna msafi bali wapo wasio na mawaa mi
naamini yapo majipu yaliyozidi na kuwa sumbufu lakini yapo yanayoanza kuiva na
yapo yasiyojulikana sasa wanaoyatumbua hao siyo majipu hivyo tuwape orodha ya
majipu yanayowahusu lakini ninong’oneze “wapi jipu lako lime kaa lilipokaa ?
nataka kulitumbua”
No comments
Post a Comment