HABARI KIMATAIFA
HABARI KITAIFA
Performance
‹
›
Cute
My Place
MICHEZO
Racing
Videos
WIZARA
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza kuiunga
mkono Polisi nchini katika operesheni ya kukamata wateja wa makahaba
kuhakikisha biashara hiyo inakoma nchini.
Tagged with: HABARI KITAIFA SIASA
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MH. UMMY MWALIMU ATAKA MADADA WANAOJIUZA NA WANUNUZI WAO KUKAMATWA
Posted by Unknown 3/09/2016 0
WIZARA
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza kuiunga
mkono Polisi nchini katika operesheni ya kukamata wateja wa makahaba
kuhakikisha biashara hiyo inakoma nchini.
Waziri wa wizara hiyo,
Ummy Mwalimu alisema takwimu zinaonesha wanawake ndio waathirika wakubwa
wa ugonjwa wa Ukimwi, ambapo kati ya Watanzania 100 wanaopimwa, sita ni
wanawake na wanaume ni wanne pekee.
Akizungumza katika
maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Dar es Salaam jana, Ummy alisema
si haki kuwakamata wanawake wanaojiuza na kuwaacha wateja wao ambao ni
wanaume.
“Ninalipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua hiyo kwa sababu
imeonesha kutoegemea upande mmoja kwa kuwakamata wanawake makahaba.
Wote wanaojiuza na wanaonunua huduma hiyo ni wakosaji wanaostahili
kuchukuliwa hatua za kisheria.Tunaungana na Polisi kushiriki operesheni
hiyo,” alisema.
Alieleza kuwa, biashara ya ukahaba inayofanywa na
wanawake isingekuwepo endapo wateja wasingekuwepo, hivyo, wateja
wanastahili kukamatwa pia kwa sababu ndio wanaoichochea.
Ummy
alisema familia nyingi zina misukosuko na wanawake wengi wamekuwa
wakiteseka na wengine kuambukizwa magonjwa na waume zao wanaoshiriki
biashara hiyo.
Katika hatua nyingine, alisema sasa wanataka kuona
idadi ya wanaume wateja wa biashara hiyo inatajwa sambamba na ya
wanawake wanaokamatwa nao ili ndugu na wake zao wafahamu kuhusu tabia
yao hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki,
alisema hatua ya kukamata wateja na wauza miili imetokana na makubaliano
yaliyofikiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Dar es Salaam.
Tagged with: HABARI KITAIFA SIASA
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments
Post a Comment