Kisiwa cha Stora Karlso nchini Sweden, ambacho ni maskani muhimu ya ndege aina ya common murre katika bahari ya Baltic.
Ili kuchunguza athari ya binadamu kwa mazingira ya asili na kuthibitisha ufanisi wa hatua ya kuhifadhi mazingira, watafiti wanahitaji kuchambua hali ya ndege hao katika miongo kadhaa hata karine moja iliyopita.
Lakini kuchambua hali yao ya zamani iliyopita si jambo rahisi, kwa sababu hali yao ilianza kurekodiwa katika miaka 30 hadi 40 iliyopita. Tunawezaje kujua hali ya zamani kabla ya hapoi?
Watafiti wametumia miaka mitano kutafuta makala, magazeti na rekodi zilizohifadhiwa katika majumba ya makumbusho, pia wamewatembelea watalii waliowahi kwenda kwenye kisiwa hiki ili kutafuta picha za kitaliiwalizopiga.
Mwishowe watafiti wamekusanya picha 113 zilizopigwa kuanzia mwaka 1918 hadi mwaka 2005, kuziweka pamoja na picha zilizorekodiwa nao kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2015, na kupata rekodi kamili ya idadi ya ndege katika karibu miaka mia moja.
Watafiti wamegundua kuwa mwanzoni mwa karne iliyopita idadi ya ndege ilikuwa ndogo sana, baadaye ilianza kuongezeka na kupungua tena katika miaka ya 60 na 70, na kuongeza tena na kufikia kiwango cha juu zaidi katika miaka ya hivi karibuni. mabadiliko hayo yanaendana na vitendo vya binadamu.
Mwanzoni idadi ya ndege ilikuwa ndogo kutokana na uwindaji wa binadamu. Hali hii ilibadilika baada ya binadamu kuanza kuhifadhi kisiwa hiki.
Katika miaka ya 60 uchafuzi wa dawa za kuwaua wadudu ulisababisha idadi ya ndege kupungua.
Na katika miaka ya hivi karibuni watu walianza kudhibiti uvuvi, ndege wanaweza kupata vyakula vya kutosha, na idadi yao imeongezeka.
Source: Chinaswahili internationali

No comments
Post a Comment