Jeshi la wanamaji wa Ufaransa linalopiga doria kaskazini mwa bahari hindi limekamata silaha kutoka kwa meli moja iliokuwa ikielekea Somalia.
Silaha hizo ni pamoja na mamia ya bunduki pamoja na silaha za kupambana na vifaru.
Hatua hiyo inajiri wiki kadhaa baada ya wanamaji wa Australia kukamata silaha nyingi zilizokuwa zikielekea Somalia.
Meli hiyo ilionekana na ndege za wanamaji wa Ufaransa ambayo ni mojawapo wa vikosi vya kimataifa vinavyopiga doria katika bahari Hindi.
Vikosi hivyo vya Ufaransa vilikamata silaha hizo chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa kuzuia silaha kutowafikia wapiganaji wa wa al-shabab.
Muungano huo wa wanamaji umepongeza kukamatwa kwa silaha hizo kama mafanikio makubwa ijapokuwa haujatoa habari zozote kuhusu wale wanaosafirisha silaha hizo.
No comments
Post a Comment