BARAZA Kuu la Waislaam nchini (Bakwata) kwa kushirikiana na Shia wamekabidhi msaada wa madawati 500 kwa serikali ili kusaidia upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Bin Zuberi amesema kuwa katika msaada hawaangalii suala la dini kinachoangaliwa ni watakaolia madawati hayo ni watanzania.
Mufti Zuberi amesema kuwa wamechangia katika kusaidia serikali kauli mbiu ya elimu bure katika kuweza kusaidia watanzania wapate elimu.
Amesema kuwa wataendelea kushawishi waislaam katika kuendelea kuchangia elimu ili watoto wapate elimu iliyo bora kwa kuwa serikali pekee yake haiwezi kutatua changamoto zote za elimu.
Mwenyekiti wa SHIA, Azim Dewj amesema kuwa amepeleka msaada huo katika bakwata ikiwa ni kuonyesha umoja na jinsi ya kusaidia serikali katika upande wa elimu.
Amesema kuwa ataendelea kushawishi matajiri wenzake kuangalia namna watakavyosaidia katika sekta ya elimu upande wa madawati kuwa kila mwaka kuweza kuchangia madawati 1000.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu amesema kuwa msaada wa madawati hayo ni mkubwa kutokana na changamoto iliyopo mbele yao.
Amesema kuwa idadi ya wanafunzi wa darasa la kwanza kuandikishwa umeongezeka kutokana na mpango wa elimu bure hivyo serikali kupata madawati ni jambo la furaha na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia madawati kutokana na mahitaji kuwa makubwa.
No comments
Post a Comment