Mripuko wa homa ya manjano umesababisha vifo vya watu wasiopungua 21 katika Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo.
Taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO), imesema kuwa baadhi ya waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo hatari walikuwa wanaishi katika mpaka wa nchi hiyo na Angola, nchi ambayo imeshudia zaidi ya vifo vya watu 200 kutokana na ugonjwa huo hadi sasa.
WHO imesema kuwa, vifo hivyo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vilitokea kati ya Januari na Machi mwaka huu, huku kesi 151 zikirekodiwa. Taarifa ya Shirika la Afya Duniani imeongeza kuwa, kuna uwezekano mkubwa maambukizi na vifo zaidi vinavyotokana na homa ya manjano vikashudiwa nchini Kongo DR.
Mapema mwezi huu, Wizari ya Afya ya Angola ilitangaza kuwa, idadi ya watu waliopoteza maisha nchini humo kwa homa ya manjano imeongezeka na kufikia 225 na kwamba hadi sasa kumeripotiwa kesi 1600 za homa hiyo.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa homa ya manjano vinatokea katika bara la Afrika.

No comments
Post a Comment