Bunge la Ugiriki limepitisha mswada wa kuwarejesha Uturuki baadhi ya wahamiaji, ambao wanakadiriwa kufikia takribani 72,000.
Makubaliano hayo yanalenga kuisaidia nchi hiyo kuwahudumia takriban wakimbizi 52,000 waliokwama nchini humo baada ya mataifa ya Balkan kufunga mipaka yake mwezi Febuari, nchi ambazo ndipo wahamiaji wanapotaka kuelekea.
Kwa mujibu wa mpango huo, mkimbizi yeyote aliyefika nchini Ugiriki kabla ya Machi 20 na kushindwa kujiandikisha ama kupata kibali kinachomruhusu kupatiwa hifadhi – atarejeshwa Uturuki.
Halikadhalika kwa kila mhamiaji ambaye Uturuki itamrejesha Syria, mhamiaji mwingine kutoka Uturuki atahamishiwa barani Ulaya kupitia njia halali na salama.
Mswada huo wa Ugiriki unafungua njia ya kuyatekeleza makubalino ya kupunguza mmiminiko wa wahamiaji barani Ulaya yaliyofikiwa baina ya Uturuki na Umoja wa Ulaya.
No comments
Post a Comment