Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo Aprili 30 ,2016 kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, klabu ya Yanga ilikuwa uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kucheza mchezo wake wa 26 wa ligi Kuu Tanzania bara na wenyeji wao Toto Africans.
Mchezo dhidi ya Toto Africans na Yanga haukuwa mchezo rahisi kwa Yanga kupata matokeo, tofauti na miaka ya nyuma ambapo kulikuwa na imani imejengeka kuwa Toto ni tawi la Yanga, kitu ambacho dhamira na uwezo wa Toto Africans waliouonesha ulidhiirisha kuwa wao sio tawi la Yanga.
Toto Africans walianza kwa jitihada na dakika ya 39 kupitia kwa William Kimanzi walifanikiwa kupata goli la uongozi, furaha ya wana Yanga ilirejea kuanzia dakika ya 50 baada ya Amissi Tambwe kuisawazishia Yanga na dakika ya 77 Juma Abdul Jafari akaipatia Yanga goli la ushindi.
Yanga wanaendelea kusalia kileleni wakiwa na jumla ya point 65 na kufuatiwa na Azam FC wenye point 58 na Simba wenye point 57, Yanga sasa imesalia na mechi nne za Mbeya City, Ndanda FC, Majimaji na Stand United ambazo zote itacheza ugenini.
No comments
Post a Comment