Bunge limepitisha bajeti ya wizara ya nishati na madini kwa mwaka wa fedha 2016/17 huku wabunge wakiitaja bajeti hiyo kama chachu ya Tanzania yenye viwanda kupatikana kufuatia uhakika wa umeme nchi nzima kuahidiwa.
Baadhi ya wabunge wamesema mipango mingi ya upatikanaji wa umeme ambayo imeelezwa katika bajeti hiyo inatekelezeka na kuwa wana imani kubwa na Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo Sospeter Muhongo katika kusimamia utekelezaji wake.
Wabunge wengine wameishauri Serikali kuboresha usimamizi wa sekta ya madini kwa kuwa bado kuna mapungufu makubwa katika usimamizi wa sekta hiyo na kama itasimamiwa ipasavyo mapato yatokanayo na sekta hiyo yataongezeka.
Kufuatia kupita kwa bajeti hiyo ambayo ni shilingi trilioni 1.22 kunatoa fursa kwa bajeti ya wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi kuweza kujadiliwa kwa siku mbili ambazo ni jumamosi na jumatatu
No comments
Post a Comment