Mchezaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya HispaniaLionel Messi na baba yake mzazi Jorge Messi wanatuhumiwa kwa kosa la ukwepaji kodi na leo May 31 2016 inaripotiwa kesi yao kuanza kusikilizwa katika jiji la Barcelona Hispania.
Messi ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara tano, anajiandaa na michuano ya Copa America itakayofanyika mwaka huu USA, lakini kesi inayomkabili ya ukwepaji kodi wa Pound milioni 3.2 ambazo ni zaidi ya bilioni 10 za kitanzania imeanza kusikilizwa.
Kiasi cha kodi wanachodaiwa Messi na baba yake, walikwepa kulipa kodi hiyo kati ya mwaka 2007 na 2009 wakati mauzo ya picha za staa huyo wa FC Barcelona, ofisi ya waendesha mashtaka wamependekeza Lionel Messi na baba yake wahukumiwe miezi 22 jela.
No comments
Post a Comment