Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa Benjamin Mkapa
Akizungumza wakati akifungua mjadala wa mazungumzo hayo rais
mstaafu bwana mkapa amesisistiza umuhimu wa pande zinazopingana kutoa ushirikiano
ili lengo la kurejesha amani nchini burundi liweze kufikiwa.
Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa
ameanza mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa burundi kwa kuzitaka
pande zinazopingana kutambua kwamba hatima ya amani ya nchi iko mikononi mwao.
Akizungumza wakati akifungua mjadala wa mazungumzo hayo huko
Arusha nchini Tanzania, rais mstaafu bwana Mkapa amesisistiza umuhimu wa pande
zinazopingana kutoa ushirikiano ili lengo la kurejesha amani nchini Burundi
liweze kufikiwa.
Hatua ya kuanza mazungumzo hayo imepokelewa kwa matumaini
makubwa na wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa akiwemo Jamar Bonomaar kutoka
umoja wa mataifa na katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki balozi Liberate
Mfumukeko ambao wamesema watahakikisha kuwa wanatoa ushirikiano mkubwa.
Hata hivyo katibu wa chama cha CNDD bwana William
Munyembabazi na mtendaji mkuu wa chama cha wanasheria wa Afrika wamesema hatua
ya baadhi ya vyama vidogo vya upinzani na wanaharakati wengine wa Burundi
kutoalikwa katika mjadala huo inaweza kuathiri mazungumzo hayo.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuendelea kwa siku nne
mfululizo .
No comments
Post a Comment