Ukimzungumzia star wa Fc Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi unamzungumzia mtu anayetajwa kuwa Mchawi wa soka ulaya, hii inatokana na uwezo wake wa kucheza soka na kuweka kambani mipir akila anapopat anafasi ya kufanya hivyo, alfajiri ya leo June 22 2016 star huyo kwa mara nyingine ameweka rekodi mpy ana ya kihistoria baada ya kuivunja ya gwiji wa soka nchini Argentina Gabriel Batistuta y akuwa mfungaji wa muda wote katika mchezo wa nusu fainali waliyoshinda na kutinga fainali ya Copa America 2016.
Lionel Messi amefanikiwa kuvunja rekodi hiyo katika timu ya taifa ya Argentina, baada y akufukisha jumla ya magoli 55 baada ya kufunga goli moja katika dakika ya 32 katika ushindi wa magoli 4-0 nusu fainali ya Copa America 2016 dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo USA.
G. Batistuta hadi anastaafu kuichezea timu ya taifa ya Argentina alifanikiwa kufunga magoli 54, rekodi ambayo imevunjwa na Lionel Messi aliyefunga jumla ya magoli 55 na kuwa ndio mfungaji bora wa Argentina wa muda wote, magoli mengine ya Argentina yalifungwa na Ezzekiel Lavezzi dakika ya 4, na Gonzalo Higuan dakika ya 50 na 86.
na hili hapa chini ndilo Goli la 55 kwa Lionel Messi lililovunja rekodi ya Gwiji Batistuta>>>>
jumla y amagoli yote y aArgentina Highlights>>>
jumla y amagoli yote y aArgentina Highlights>>>
No comments
Post a Comment