KIKAO
cha Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Coastal Union kilichoketi juzi kwa
saa tatu kilitoka na mapendekezo wa kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa
timu hiyo,Jackson Mayanja kutokana na kutokuwepo kwa mwenendo wa matokeo
mazuri kwa timu hiyo tokea alipokabidhiwa.
Alisema kuwa sababu kubwa zilizopelekea kuachana na kocha huyo zinatokana na aina ya ufundishaji wake kutokuendana na kasi ya timu hiyo kutokana na wachezaji kukosa stamina hali iliyopelekea kushindwa kucheza kwa mafanikio kwenye mechi zao.
Kocha
Mayanja alikabidhiwa kikosi hicho cha Wagosi wa Kaya baada ya
kumalizika msimu wa ligi kuu uliopita akichukua mikoba ya Jamhuri
Kihwelu “Julio” ambaye aliinusuru timu hiyo na kushuka daraja ikimaliza
ikiwa nafasi tano za juu kwenye msimamo.
mara
baada ya kumalizika kikao hicho,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar
Assenga alisema kuwa kikao hicho kilikutana chini ya Mwenyekiti wao
Dr.Ahmed Twaha ambapo pamoja na mambo mengine kilikuwa na agenda kadhaa
lakini kubwa ikiwa sababu za timu hiyo kutokufanya vizuri kwenye
michuano ya Ligi kuu.
Assenga
alisema kuwa agenda hiyo ilikuwa mzito kwa wajumbe kutokana na timu
usajili makini uliofanywa kwa wachezaji lakini wakaonekana kushindwa
kuendana na kasi iliyokuwa ikitakiwa ili kuweza kuipa mafanikio timu
hiyo kwenye mechi zao.
Alisema kuwa sababu kubwa zilizopelekea kuachana na kocha huyo zinatokana na aina ya ufundishaji wake kutokuendana na kasi ya timu hiyo kutokana na wachezaji kukosa stamina hali iliyopelekea kushindwa kucheza kwa mafanikio kwenye mechi zao.
“Lakini hata ukiangalia wakati wa mazoezi wachezaji wetu wamekuwa
wakichezeshwa nusu uwanja huku kwenye mechi za ligi kuu wanatakiwa
kucheza uwanja mzima pamoja na timu yetu kupoteza stamina na wachezaji
kupoteza umakini kutokana na aina ya ufundishaji wake,”Alisema
Aidha
alisema kuwa baada ya mechi ya leo(jana) timu hiyo itakuwa chini ya
Mbwana Bushiri Akisaidiana na Kamati ya Ufundi ya timu hiyo ambao
watakuwa na jukumu la kuiandaa timu hiyo kuelekea mapambano ya Ligi kuu
soka kwenye mechi zinazofuata.
Hata
hivyo alisema kuwa tayari Mwenyekiti wa timu hiyo,amemuagiza Katibu
Mkuu wa timu hiyo,Kassim El Siagi kuwaandikia barua Kamati ya Ufundi
haraka iwezekanavyo ili waweze kutambua majukumu yao hayo mpaka
atakapopatikana Kocha Mpya.
No comments
Post a Comment