Baad
ya kulazimishwa sare ya kufungana kwa goli 1-1 na Azam FC, Yanga
wameendeleza wimbi lao la ushindi kwa kuitandika timu ya Toto Africans
ya jijini Mwanza kwa goli 4-1 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa taifa.
Beki
wa kulia wa Yanga Juma Abdul aliifungia Yanga goli la kuongoza dakika
ya tisa kipindi cha kwanza kwa kupiga shuti akiwa nje ya eneo la hatari
na mpira huo kujaa moja kwa moja wavuni.
Goli
hilo lilidumu kwa kipindi chote cha kwanza ambapo Toto Africa
walionekana kuzidiwa kwa kiasi kikubwa kwenye eneo lao la katikati.
Yanga
walirudi kipindi cha pili wakiwa wamecharuka na kuongeza goli la pili
dakika ya 48 mfungaji akiwa ni Simon Msuva. Wakati dakika zikiwa
zinayoyoma, mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi Amis Tambwe akaifungia
Yanga goli la tatu dakika ya 81.
Wakati
dakika zikiwa zinakaribia kumalizika, Simon Msuva alifunga bao la nne
lakini likiwa ni goli la pili kwa upande wake na kuifanya Yanga iondoke
uwanjani kwa ushindi wa goli 4-1.
Golikipa
wa Toto Africans Mussa Mohamed alidaka penati iliyopigwa na
mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma baada ya beki wa Toto kuunawa mpira
kwenye eneo la hatari akiwa katika harakati za kuokoa hatari kwenye
lango lao.
Goli pekee la kufutia machozi kwa upande wa Toto Africans limefungwa na Miraji Athumani kipindi cha pili.
No comments
Post a Comment