Baada
ya kuifunga timu ya Mbeya City, Wekundu wa Msimbazi wameshindwa kutamba
leo kwenye uwanja wa Sokoine mbele ya Tanzania Prisons kufuatia kupokea
kichapo cha goli 1-0 mchezo uliomalizika jioni ya leo.
Goli pekee na la ushindi kwa upande wa Tanzania Prisons ‘wajelajela’ limekwamishwa wavuni na Mohamed Mkopi katika dakika ya 62.
Mwamuzi wa mchezo wa Tanzania Prisons dhidi ya Simba akimzawadia kadi ya njano James Mwasoke |
Ushindi
huo unakuwa ni wanne kwa Prisons ambayo imeshinda michezo mitatu
nyumbani huku ushindi wake wa ugenini ukiwa ni dhidi ya Kagera Sugar
walioibuka na ushindi mnono wa goli 3-0 kwenye uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi, Tabora.
Mwishoni
mwa juma lililopita Simba ilifanikiwa kushinda kwa mara ya kwanza mbele
ya Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya tangu timu hiyo ilipopanda
daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara.
Kufungwa
kwa Simba leo hii, kunawafanya wawe wamepoteza mchezo wa pili msimu
huu, mchezo wao wa kwanza kupoteza ulikuwa ni ule dhidi ya watani wao wa
jadi Yanga uliopigwa Septemba 26 mwaka huu.
No comments
Post a Comment