Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Judith Mwangi ‘Avril’ ambaye alicheza kama video queen kwenye wimbo wa Diamond Platnumz ‘Kesho’ amefunguka na kusema hakuwahi kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz kama ambavyo baadhi ya watu walivyokuwa wakidhani huenda kuwa Diamond Platnumz baada ya video hiyo labda alitumia nafasi hiyo kutoka naye kimapenzi.
Avril alisema kuwa yeye na Diamond Platnumz hawakufanya project nyingine yoyote zaidi ya kutengeneza video ile ya ‘Kesho’ japo alimuelezea Diamond kuwa ni msanii mpole sana na mwenye kupenda kazi yake na kujituma.
“Diamond ni rafiki yangu ni mtu poa sana, tumejuana kwa muda mfupi lakini ni msanii mwenye bidii ya kufanya kazi na kukutana na msanii mwenye bidii ni jambo zuri, hi mtu mzuri mpole hana maneno na watu. Najua vyombo vya habari vinampa sifa nyingi tofauti na yeye lakini ukikutana na yeye moja kwa moja ni mtu mzuri sana. Baada ya kufanya ile video ya kesho hakuna project nyingine tulifanya” alisema Avril
Mbali na hilo Avril alitaja wasani watano kutoka Tanzania ambao anawakubali na kuanza na Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz, Raymond, Vanessa Mdee pamoja na Linah Sanga.
No comments
Post a Comment