Kumekuwa na taarifa juu ya kijana mmoja Mtanzania aliyeteswa hadi kufa katika machimbo ya Nyamhuna Mkoani Geita, taarifa hizi zimerushwa sana hasa picha zake katika mtandao wa kijamii pamoja na baadhi ya vyombo vya habari.
suala hilo likamfanya Waziri wa mambo ya ndani wa nchi Mh.Mwigulu Nchemba kuingilia kati na kufika mwenyewe mkoani Geita na kujionea kila kilichoendelea.
hii ndi kauli yake na alichoamua.........
"Nimefika Mgodi wa Nyamhuna unaodaiwa kuwa raia wa china ambao ni sehemu ya wamiliki wa mgodi huo wakishirikiana na watanzania walimtesa kinyama na kumjeruhi mmoja wa mtanzania mwenzetu aliyekuwa akifanya kazi katika mgodi huo uliopo Katoro-Geita".
"Imenilazimu kufika gereza la Geita kukutana na kijana huyo ambae yupo hai tofauti na taarifa za awali kuwa alifariki".
"Baada ya kujiridhisha kuanzia mavazi,majeraha,picha,sura na umbo lake kuwa ndiye kijana aliyeteswa vibaya na picha zake kusambaa mitandaoni na vyombo mbalimbali vya habari,niliamua kwenda naye hadi mgodini lilipofanyika tukio hilo la kinyama,aliwatambua wahusika ambao NI KWELI WALIFANYA TUKIO HILO LA KINYAMA NA LISILOKUBALIKI HAPA NCHINI".
"Hivyo walioshiriki tukio hilo tumeshawashikilia kupitia jeshi la polisi tayari kwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria".
"Nalaani tukio hilo vikali sana,serikali hii ipo tayari kushirikiana na kila mmoja rai mwema kutoa taarifa popote pale za matukio au viashiria viovu na vinavyohatarisha usalama wetu".
Mchina akimhadhibu kijana huyo kama unavyoshuhudia hapo, ni picha iliyozagaa sana mitandaoni |
No comments
Post a Comment