Jana
July 23 2016 Rais John Pombe Magufuli alikabidhiwa rasmi nafasi ya
uenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM baada ya kupigiwa kura za ndio
2398 kutoka kwa wanachama wa chama hicho ambapo hakuna kura hata moja
ya hapana wala iliyoharibika
Baadhi
ya viongozi wakiwemo wa vyama vya upinzania walishiri akiwemo
mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema, lakini wapo pia waliotamani kufikisha
hisia zao kuhusu tukio hilo na mmojawapo ni mbunge wa Kigoma mjini
Zitto Kabwe kupitia account yake ya facebook aliandika maneno haya…
"Napenda
kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa
Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama hicho. CCM imeendelea
kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila baada ya muda
"Jambo
ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na barani
Afrika. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa
Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa
Sheria za Nchi yetu.
"Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais." –Zitto Kabwe
No comments
Post a Comment