Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara zake za
utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika
kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi, Kaskazini na
ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.
Mhe. Lukuvi kwa siku ya jumatatu
tarehe 19 Desemba 2016 atatua migogoro ya ardhi ya wilaya ya Musoma
mkoani Mara na siku ya jumanne tarehe 19 Desemba 2016 atatua migogoro ya
ardhi ya wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi
atakutana na wananchi wa Musoma mjini na wananchi wa Bunda walio na kero
za migogoro ya ardhi na kuzitatua pamoja na kutembelea miradi
inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika wilaya ya
Musoma.
Aidha, Mhe. Lukuvi baada ya ziara
hiyo anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha ambapo pia atatua migogoro ya
ardhi inayoukabili mkoa huo.
Hadi sasa Mhe. Lukuvi ndani ya
mwezi huu wa Desesmba ameishatatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Kigoma
na wilaya zake za Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa wa
Shinyanga na wilaya zake za Kishapu na Shinyanga mjini na katika mkoa wa
Geita amefanya ziara katika wilayani Chato.
No comments
Post a Comment