Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya Kimataifa ya Mitandao ya Kisasa
ya Mawasiliano ya ZTE ya Mji wa Shengzhen Nchini Jamuhuri ya Watu wa
China zimetiliana saini Mkataba wa ushirikiano katika uendelezaji wa
miradi itakayotumia mfumo unaokubalika Kimataifa kwa hivi sasa.
Miradi
hiyo itakayotumia mfumo waTeknolojia ya Kisasa { TEHAMA } ni pamoja na
Mradi wa Mawasiliano Serikalini { E Goverment } huduma za umeme,
usafiri, miji mipya, afya pamoja na huduma za Kijamii ikiwemo utaratibu
wa udhibiti wa ukusanyaji wa Mapato ya Serikalini.
Saini
ya Mkataba huo imetiwa na Rais wa Kampuni ya ZTE Bwana Zhang Rejun
wakati upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiwa na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye yuko Nchini China
kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku Tano.
Akizungumza
na Uongozi wa Kampuni hiyo ya ZTE kwenye Makao Makuu yake Mjini
Shengzhen Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Zanzibar inaendelea kuipa fursa zaidi Kampuni ya ZTE katika
mtazamo wake wa miradi ya maendeleo inayotarajia kuanzisha hapo baadaye.
Balozi
Seif alisema hatua hiyo ya Serikali imekuja kutokana na Uongozi wa juu
wa Kampuni ya ZTE kuonyesha juhudi kubwa za kuendelea kuunga mkono
harakati za kuimarisha miradi ya Maendeleo zinazotekelezwa na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliishukuru na kuipongeza Kampuni ya ZTE
kwa kasi kubwa ya uwajibikaji wa watendaji wake katika mfumo wa
Teknolojia ya kisasa ya mawasiliano unaoonekana kukubalika na Mataifa
mengi Duniani zikiwemo pia Nchi za Bara la Afrika.
Balozi
Seif aliutolea mfano mradi Mkubwa wa mawasiliano Serikalini {E
Goverment } ambao ulisimamiwa na Kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar
ukikamilika katika awamu ya kwanza.
Naye
Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d alisema
kazi kubwa inayofanywa na Uongozi wa Kampuni ya ZTE katika kusaidia
miundombinu ya mawasiliano Zanzibar imeleta faraja kwa Wananchi walio
wengi Visiwani Zanzibar.
Dr.
Khalid alisema wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikijitahidi
kuendelea kudhibiti mapato yake kwa kutumia mfumo wa Kisasa wa
Mawasiliano Kampuni ya ZTE bado ina nafasi ya kusaidia Taaluma katika
kazi hiyo kwa lengo la kupata ufanisi mkubwa zaidi.
Mapema
Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Mitandao ya Kisasa ya Mawasiliano ya
ZTE ya Mji wa Shengzheng Nchini China Bwana Zhang Rejun aliueleza Ujumbe
wa Zanzibar unaoongozwa na Balozi Seif kwamba Kampuni yake hivi sasa
tayari imeshatekeleza miradi ipatayo Mitano Visiwani Zanzibar.
Bwana
Zhang alisema uwamuzi wa Uongozi wa Kampuni yake kuongeza Miradi
Zanzibar umekuja kutokana na mazingira bora ya uwekezaji pamoja na
rasilmali za asili za maumbile zilizotoa kigezo kikubwa kwa Kampuni
hiyo.
Kampuni
ya Kimataifa ya Mitandao ya Kisasa ya Mawasiliano ya ZTE ya Mji wa
Shengzheng Nchini iliyoasisiwa mwaka 1985 tayari imeshawekeza miradi
yake katika Mataifa 60 ulimwenguni na kupata tuzo tofauti katika ubora
wa utoaji huduma zake katika kiwango kinachokubalika Kimataifa.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments
Post a Comment