YANGA SC
Kikosi cha Yanga
kimerejea nchini baada ya kupoteza mechi yake ya tatu ya Kombe la Shirikisho
dhidi ya Medeama nchini Ghana.
Yanga wametua
nchini kwa mafungu, wakianza na kundi la kwanza lililotua jijini Dar es Salaam
saa 8 usiku.
Baadaye saa 2
asubuhi, kundi la pili likiongozwa na kocha Hans van der Pluijm nalo
likawasili.
Ingawa mashabiki
wamekuwa wakijaribu kujipa moyo, lakini hali halisi hasa ni kwamba Yanga haina
nafasi tena ya kufuzu hatua ya nusu fainali.
Kocha Pluijm,
amesisitiza makosa ambayo waliyazungumza, yamefanyika na kuwafanya wapoteze
mchezo.
Ingawa alilalamika
suala la safari ndefu hasa ile ya basi baada ya kuwa wamewasili Ghana.
SIMBA SC
Viongozi
na wanachama mbalimbali wa Simba watachangia damu katika hospitali mbalimbali.
Rais
wa Simba, Evans Aveva amesema watafanya hivyo ikiwe ni sehemu ya kuadhimisha
wiki ya Simba kwenda kusherekea miaka 80 ya klabu hiyo.
Siku
kamili ya sherehe itakuwa ni Agosti 8 wakati tamasha la Simba Day
litakapofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijiji Dar es Salaam.
Kocha Zdravko
Logarusic anarejea jijini Dar es Salaam, safari hii akiwa amepewa kazi ya
kukipima kikosi cha Simba.
Logarusic maarufu kama
Loga, anakuja nchini ndani ya siku chache akiwa ameongozana na kikosi chake cha
Inter Club cha Angola.
Kikosi hicho
kitapambana na Simba katika mechi ya Simba Day ambayo itapigwa Agosti 8, siku
ambayo Simba itauwa inatimiza miaka 80.
Tayari Logarusic
alikuwa amesema angetamani kukutana na Simba na kuwaonyesha kazi yake ilivyo
bora.
Sasa Simba inanolewa na Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon na imejichimbia mjini Morogoro.
Chini ya kocha huyo,
Simba imecheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Polisi Morogoro iliyo daraja la
kwanza na kuivurumisha kwa mabao 6-0.
AZAM FC
Mshambuliaji
raia wa Zimbabwe, Brian Abbas Amidu ametua nchini tayari kujaribiwa katika
kikosi cha Azam FC.
Amidu amesafirishwa hadi mjini Zanzibar ambako Yanga imeweka kambi yake kujiandaa na Ligi kuu Bara msimu mpya wa 2016-17.
Azam
FC inahaha kupata straika kwa kuwa mshambuliaji wake Kipre Tchetche amegoma
kurejea nchini.
KIMATAIFA
TP MAZEMBE
Wakati
Yanga ya Tanzania imepoteza matumaini kabisa ya kusonga mbele hatua ya nusu
fainali ya Kombe la Shirikisho, TP Mazembe, leo wamejihakikishia nafasi hiyo.
TP
Mazembe imeilaza Mo Bejaia kwa bao 1-0 katika mechi iliyopigwa mjini
Lubumbashi, mfungaji akiwa Rainford Kalaba katika dakika ya 61.
Kwa
ushindi huo, Mazembe imefikisha pointi 10 ambazo zinaipa uhakika kubaki katika
nafasi ya kwanza au ya pili kulingana na matokeo ya mechi mbili zilizobaki kwa
kila timu ya Kundi A.
Bejaia wana mechi mbili, dhidi ya Yanga ugenini na Medeama nyumbani wakati TP Mazembe mbili zao, moja ni ugenini dhidi ya Medeama na nyumbani dhidi ya Yanga.
Kama itashinda mechi nyingine moja kati ya hizo mbili, TP Mazembe itakuwa imejihakikisha kukaa kileleni mwa kundi hilo.
Kwa muonekano, Mo Bejaia iliyo katika nafasi ya pili na Medeama nafasi ya tatu, kila moja ina nafasi kwa kuwa kila moja ina pointi tano.
Lakini uwezekano wa kufuzu unabaki kwa moja kwa kuwa zitakutaka. Kama zitatoka sare, zitakuwa zimeipa nafasi Mazembe kubaki kileleni lakini moja ikishinda, itakuwa imepata nafasi na moja kupoteza.
Bejaia watataka kushinda mechi dhidi ya Yanga jijini Dar es Salaam, ili mechi ya mwisho dhidi ya Medeama iwe fainali. Lakini Medeama nayo italazimika kuilaza Mazembe ugenini ili iwe isubiri mechi ya mwisho.
Kwa kifupi, sasa ushindani wa nafasi moja umebaki kwa Bejaia na Medeama huku Yanga ikiwa imeaga rasmi.
Bejaia wana mechi mbili, dhidi ya Yanga ugenini na Medeama nyumbani wakati TP Mazembe mbili zao, moja ni ugenini dhidi ya Medeama na nyumbani dhidi ya Yanga.
Kama itashinda mechi nyingine moja kati ya hizo mbili, TP Mazembe itakuwa imejihakikisha kukaa kileleni mwa kundi hilo.
Kwa muonekano, Mo Bejaia iliyo katika nafasi ya pili na Medeama nafasi ya tatu, kila moja ina nafasi kwa kuwa kila moja ina pointi tano.
Lakini uwezekano wa kufuzu unabaki kwa moja kwa kuwa zitakutaka. Kama zitatoka sare, zitakuwa zimeipa nafasi Mazembe kubaki kileleni lakini moja ikishinda, itakuwa imepata nafasi na moja kupoteza.
Bejaia watataka kushinda mechi dhidi ya Yanga jijini Dar es Salaam, ili mechi ya mwisho dhidi ya Medeama iwe fainali. Lakini Medeama nayo italazimika kuilaza Mazembe ugenini ili iwe isubiri mechi ya mwisho.
Kwa kifupi, sasa ushindani wa nafasi moja umebaki kwa Bejaia na Medeama huku Yanga ikiwa imeaga rasmi.
ASENAL WENGER
Meneja wa Arsenal Arsene
Wenger kuna uwezekano wa kukiacha kiti chake hicho cha umeneja kwa kocha wa
kikosi cha Bournemouth Eddie Howe, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Daily
Star.
Taarifa zinadai kuwa
Arsenal itakuwa sawa na mashabiki wengi watafurahi kumuona wenger akichomoka
katika kikosi hicho baada ya majira ya joto kikosi hicho kilipoanza kumtafuta
kocha mpya atakayemrithi mfaransa huyo aliyeingia katika kipindi cha miezi kumi
na mbili ya mwisho ya mkataba wake.
ROGERS CUP
Mwana dada huyo amefikia hatua hiyo kwa ushindi wa 7-5 6-1 dhidi ya
King.
Johanna Konta ambaye katika uchezaji Duniani yuko kwenye nafasi ya 14,
katika hatua inayofuata atakutana na Mmarekani Varvara Lepchenko
BALOTELI
hatimae Klabu ya Hull City ya Uingereza
imemsajili Mario Balotelli kutoka Liverpool kwa pauni milioni 26.
Hii imekuwa taarifa njema kwake kwani
Liverpool haikuwa imempanga kucheza msimu huu.
Hata hivyo wachezaji mahiri wa soka kama kama
vile Adrea Pirlo Wamesikitishwa na kushangazwa na kudorora kwa soka la
Balotelli.
CARLOS TEVEZ
Star wa Boca Juniors
star na straika wa zamani wa Manchester city,Manchester united na Juventus Carlos Tevez amefichua kwamba
alipigiwa simu na kocha wa chelsea Antonio Conte akimpa ofa ya kuichezea klabu
ya Chelsea.
Mshambuliaji huyo wazamani wa Juventus alikuwa akitarajia kutwaa kombe
la pili la Copa Libertadores akiwa na Boca lakini timu yake iliishia nusu
fainali baada ya kupoteza mbele ya klabu ya Independiente del Valle.
Tevez amethibitisha kwamba Conte,ambaye ni kocha wake wa zaman akiwa
juventus alimpa ofa hiyo iliyolenga kumrejesha Ulaya kwa mara nyingine lakini
alikumbuka kwamba tayari alishastaafu soka la kimataifa na kuamua kuendelea
kuchezea nyumbani kwao Argentina.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32-akizungumza na Radio La Red ya huko kwao anasema kuwa
alikuwa akiendesha gari akiwa na familia yake, ambapo konte alimpigia simu na
kumwambia kuwa alikuwa akiitaji forward na kumuuliza iwapo anaweza kucheza Chelsea.
International - Champions Cup:: North America
results
Chelsea 1 - 0 Liverpool
Mfungaji- Gary
Cahill 10'
1 - 0
70' Cesc
Fabregas-straight red card
AC Milan ft
Bayern Munchen 5-3 penalties after 3-3 =90’
PSG FT Real Madrid
3-1
No comments
Post a Comment