1.LOWASA NI TISHIO
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo maarufu ‘Mzee wa Upako’ amesema kitendo cha viongozi wa CCM kulitaja zaidi jina la Edward Lowassa katika Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho ni ishara kuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani ni tishio.
“Nani! Lowassa…. jina lake kutajwa sana katika vikao vya CCM. Hiyo inaashiria kuwa ni mtu tishio. Ndiyo ni tishio,” alisema Lusekelo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Lusekelo ambaye hivi karibuni, Rais John Magufuli alishiriki ibada katika kanisa lake, alimzungumzia Lowassa baada ya kuulizwa swali juu ya mtazamo wake kuhusu Mkutano Maalumu wa CCM ambao jina la mgombea huyo wa urais kupitia Chadema na Ukawa lilitajwa na makada wengi wa chama hicho tawala.
Chanzo-Mpekuzi huru
2. MEYA MJI WA DODOMA "TUWAENZI MASHUJAA KWA KUFANYA KAZI'
Mstahiki Meya wa mji wa Dodoma Jaffari Mwanyemba, amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuwaenzi Mashujaa waliopigana katika vita mbalimbali ikiwa ni katika harakati za kuiletea uhuru nchi ya Tanzania.
Hayo yamesemwa leo saa sita usiku, wakati alipokuwa akizima Mwenge wa uhuru uliowashwa jana Julai 24, na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mheshimiwa Christina Mndeme katika kilele cha mnara wa mashujaa mnano saa 6 kamili usiku ikiwa ni sehemu ya maombolezo ya kumbukumbu ya Mashujaa, yaliyofanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo mjini Dodoma.
Chanzo: Fullshangwe
3. ANAYEINGIZA MILIONI 7 KWA DAKIKA APEWA KESI MPYA KISUTU
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo inatarajiwa kuwapandisha kizimbani wafanyabiashara wawili akiwemo Mohamed Mustafa Yusufali ‘Choma’ aliyewahi kutajwa kuwa anajipatia Sh milioni saba kwa dakika moja kwa njia za udanganyifu katika mapato ya serikali.
Choma na mfanyabiashara wa Arusha, Samweli Lema, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana saa 9 mchana kwa ajili ya kusomewa mashitaka yanayowakabili, lakini ilishindikana kwa sababu muda ulikuwa umekwisha.
Chanzo: Mpekuzi huru
KIMATAIFA
4.19 WAPOTEZA MAISHA KITUO CHA WALEMAVU JAPAN
Watu 19 wameuawa nchini Japan baada ya mtu mmoja kuwashambulia watu kwa kisu katika kituo kimoja cha walemavu, kilichoko katika mji wa Sagamihara, magharibi mwa mji mkuu Tokyo. Watu zaidi ya 20 wamejeruhiwa, wengi wao vibaya.
Ripoti nchini Japan zinasema kuwa mtu mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi katika kituo hicho cha Tsukui Yamayuri-en, alijipeleka hadi kituo cha polisi na kukiri kuwa ndiye aliyetekeleza mauaji hayo ya kutisha na kwa sasa anazuiliwa.
Chanzo: Bbcswahili.com
5. MTOTO APOTEZA MAISHA BAADA YA KUCHANGANYA MITUNGI YA GESI HUKO AUSTRALIA
Katika tukio la kuhuzunisha mtoto mmoja amepoteza maisha na mwingine mmoja kuathiriwa baada ya kufanyika uzembe katika hospitali ya Southwestern Sydney iliyopo katika jimbo la New South Wales, Australia.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Waziri wa Afya wa New South Wales, Julian Skinner alithibitisha kuwa ni kweli kumetokea tukio hilo na kutumia fursa hiyo kuomba radhi kwa niaba ya serikali ya jimbo hilo.
6. MACHAR APINDULIWA SUDAN KUSIN
Maafisa wa serikali ya Sudan Kusini wameiambia BBC kwamba wanamtambua waziri wa madini Taban Deng Gai kuwa makamu wa kwanza wa rais akichukua mahala pake Riek Machar ambaye alitoroka mji mkuu wa Juba baada ya mapigano makali mapema mwezi huu.
Hatahivyo msemaji wa Machar amesema kuwa wameukataa uteuzi wa Bwana Deng.
Bwana Deng alikuwa mpatanishi mkuu wa Machar na hatua yake ya kuchukua wadhfa huo unaonyesha kuwa wametofautiana, hivyobasi kuweka mgawanyiko katika upinzani ambao unazidi kutatiza juhudi za kupata amani nchini Sudan Kusini ,kulingana na wachanganuzi.
No comments
Post a Comment