Najib Razak, waziri Mkuu wa Malaysia
sheria ya usalama katika majeshi nchini Malaysia ambayo inampa nguvu zaidi Waziri Mkuu ,Najib Razak ,sheria hiyo itamruhusu waziri Najib kutoa tamko la eneo lolote nchini humo kuwa ni eneo la majeshi ya usalama na katika hali hiyo kumuongezea nguvu mpya ya udhibiti wa mambo nchini humo.
Na katika eneo hilo, polisi wanakuwa na uwezo wa kupekua watu,magari na hata makaazi ya watu bila ya vibali vya upekuzi.
Najib akiitetea sheria hiyo anadai ina lengo la kupambana na ugaidi, ingawa kwa upande mwingine raia wa nchi hiyo wameingiwa na hofu kwamba huenda sheria hiyo ikatumika kuwaziba midomo wapinzani wa serikali nchini humo.
Sheria hiyo imekuja wakati ambapo waziri Najib anakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka katika mataifa ulimwenguni wakitaka uchunguzi wa kina ufanywe dhidi ya udanganyifu wa fedha uliofanywa na serikali yake katika mfuko wa fedha ambao yeye anaudhibiti.
No comments
Post a Comment