Msanii mkali wa Singeli Sholo Mwamba ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo mpya wa Professor Jay amefunguka na kusema yeye hana tofauti na msanii mwenzake wa singeli Man Fongo ambaye hivi sasa anatamba na ngoma kama 'Hainaga ushemeji' .
Sholo Mwamba akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) alisema kuwa kwa sasa yeye na Man Fongo ni washindani tu katika kazi ila hana utofauti naye kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidhania.
"Mimi sina tofauti na Man Fongo, unajua Man Fongo ni mdogo wangu kabla ya kuanza kuimba na kufahamika alikuwa na 'Dj' wangu lakini baadaye alianza kuimba na kuamua kutoka yeye mwenyewe, sina tofauti na yeye kabisa sema mimi nachukulia changamoto katika kazi baada ya yeye kuanza kufanya vizuri" alisema Sholo Mwamba.
Mbali na hilo Sholo Mwamba alisema kuwa muziki wa Singeli upo na utaaendelea kuwepo kwa kuwa watu saizi wanaupenda, amesema hata kama usipochanganywa na aina nyingine ya muziki bado Singeli itabaki pale pale kama ilivyokuwa mwanzo.
No comments
Post a Comment