Timu ya mpira wa miguu ya Wanarambaramba Azam Fc imeeleza kuwa imejipanga vizuri katika kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wao wa kuwania Ngao ya Jamii watakapokutana kuchuana vikali dhidi ya timu ya Dar es salaam Young Africans – (YANGA) hapo kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu na hii ni kutokana na mazoezi na mipango mipya katika timu hizo mbili ambazo zimekuwa zikikutana na kukamiana katika michezo yao.
Akizungumza mapema leo, Msemaji wa timu ya Azam Fc, Bwana. Jaffar Iddi Maganga amesema kuwa mbali na mabadiliko ya kimfumo wa kiungozi katika timu hiyo wapo tayari na wamejiandaa vizuri kupambana na Yanga hapo kesho
“Azam FC imefanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi, kutoka kwenye uongozi wa kiingereza wa Koha Stewart na jopo lake na kuja kwa Wahispania Zebensul Rodriguez na msaidizi wake” amesema Maganga
Ameongeza Kuwa: “Wachezaji wamekua katika mtihani mgumu wa kutoka kwenye mfumo mwingine na kufata mfumo mwingine wa kimichezo, lakini kikubwa ni kwamba wachezaji wameweza kuadapt vizuri mafunzo yake” ameongeza Maganga.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).
No comments
Post a Comment