Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi amekubali kurejea katika kikosi cha timu yake ya taifa ya Argentina.
Messi alitangaza kustaafu mwezi Juni baada ya michuano ya Copa America walipofungwa na Chile.
Lakini mazungumzo yaliyohusisha hadi serikali ya Argentina, yalikuwa yakiendelea na mwisho ametangaza kwamba anarejea.
“Nilianza kuona mimi ni kama tatizo. Ninaipenda sana nchi yangu, ninaipenda sana timu yangu ya taifa,” alisema Messi.
“Ninaona ninaweza tena kuungana nao na kufanya kila juhudi ifanye vizuri, niliamua vile kwa kuwa sikutaka kuendelea kuumia au kuwaumiza wanaonitegemea,” aliongeza.
Ingawa hajasema moja kwa moja lakini inaelezwa ataanza kuitumikia tena Argentina katika mechi dhidi ya Uruguay halafu Venezuela kuwania kucheza Kombe la Dunia.
No comments
Post a Comment